
“Tuliopinga
wizi wa madini yetu tulibezwa, tulikamatwa kama wezi; tuliswekwa ndani,
tulionekana wasaliti. Leo kiko wapi? #NasimamaNaRaisWangu” aliandika Dk. Kigwangalla huku watu mbalimbali wakitoa maoni yao.
Kwa
mujibu wa Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, suala la kupambana na
rasilimali za Taifa alilianza miaka mingi kwani miongoni mwa matukio
makubwa ni la 2013, ambapo alijitolea kupambana kudai haki tukio
lililopelekea kutiwa nguvuni na Jeshi la Polisi.
Dk.
Kigwangalla anasema katika kupigania maslai Taifa ataendelea kuunga
mkono juhudi za Rais Dk. Magufuli mwanzo mwisho kwani ni moja ya
matunda ya nchi yoyote ile Duniani.
Anasema
kiongozi Mkuu lazima alinde na kupigania rasilimali za nchi, hivyo
akiwa Mtanzania na kiongozi mwenye dhamana anaunga juhudi hizo bila
kuchola.
Tuliopinga wizi wa madini yetu tulibezwa, tulikamatwa kama wezi; tuliswekwa ndani, tulionekana wasaliti. Leo kiko wapi? #NasimamaNaRaisWangu pic.twitter.com/RClqLxmtDW
— Dr. Kigwangalla, H. (@HKigwangalla) June 19, 2017
0 comments:
Chapisha Maoni