Mwenyekiti
wa CHADEMA, Mbowe amethibitisha shamba lake kuvamiwa na viongozi wa
serikali ya Wilaya na kuharibiwa miundombinu ya shamba hilo huku akidai
anajua yote hayo yanafanyika kutokana na misimamo yake ya kisiasa na
kudai hawawezi kumbadili.
Freeman Mbowe amesema hayo leo kupitia mitandao yake ya kijamii huku akikiri wazi kuwa siku ya Alhamisi ya tarehe 7 mwaka huu walipokea barua kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira -NEMC ambayo ilikuwa inadai kilimo wanachofanya kilikuwa kinaharibu mazingira hivyo hawapaswi kuendelea na kilimo hicho.
"Ni
kweli nimepata taarifa ya kuwa mkuu wetu wa wilaya ya Hai, akiambatana
na askari wa mgambo akiambatana na watu wengine ambao sijaweza
kuwafahamu wakiwemo vile vile waandishi wa habari, walikwenda kwenye
mradi wetu wa Kili Vegies ni mradi wa kilimo cha kisasa cha mboga mboga
(Green house), tukilima mboga na matunda, tukilima mboga kwa sababu ya
'local market' na wakaanza kuharibu miundombinu, ikiwemo kuharibu 'Green
houses', kukatakata mabomba , kuharibu mimea na uharibifu mwingine
mwingi" alisema Mbowe n kuongeza;
"Ni
kweli tulipokea barua ya NEMC siku ya Alhamisi tarehe 7, iliandikwa
tarehe 7 lakini tuliipata tarehe 8, tulijibu hiyo hoja ya NEMC, kwamba
tunaamini wamekosea sheria kwa sababu kilimo chetu hakiharibu mazingira
wala shutuma zilizotolewa kwamba ni kwenye chanzo cha maji sio kweli,
wanadai kwamba shamba hilo limeanzishwa kwenye chanzo cha mto Weruweru
jambo ambalo sio kweli, mto unaoitwa Weruweru unaanzia mlimani kabisa
National Park Kilimanjaro"
Mbowe
anasema kitendo hicho kilichofanywa na viongozi hao ni kitendo cha
kufedhehesha na cha kukatisha tamaa hivyo anasikitishwa sana na kitendo
hicho, huku akisema anatambua kuwa yote hayo anayofanyiwa ni kutokana na
misimamo yake kisiasa, na misimamo ya chama anachokiongoza.
"Najua
haya yanatokea kwa sababu ya misimamo yangu ya kisiasa kwa sababu wa
muelekeo wangu wa kisiasa na uthabiti na uimara wa chama
ninachokiongoza, sasa mimi siwezi kuwa kondoo, nimesema siku zote, haya
mambo ya duniani anayeyalipa ni Mungu,hawatabadilisha mawazo yangu kwa
kuharibu mali zangu, wanaweza kuharibu zote hata wakitaka roho yangu
waichukue, waichukue tu lakini haitanisababisha nibadili msimamo wangu
katika kuamini ninachokisimamia, ninachokipigania katika Taifa"
alisisitiza Mbowe
Mbali
na hilo kiongozi huyo amedai kuwa hakuna wingi wa mali zake zinaweza
kuharibiwa zikamfanya yeye akapige magoti kama watu wengine
wanavyofanya, anadai yeye hawezi kupiga magoti bali atasimama kwenye
ukweli na haki siku zote.
Hili
ni tukio la pili kwa mwaka huu kutokea kwenye shamba hilo, mwezi wa
kwanza mwaka huu serikali ilimtaka kiongozi huyo kusimamisha kilimo
kwenye shamba hilo ikidai kuwa lipo kwenye chanzo cha maji.
0 comments:
Chapisha Maoni