Bunge
limeitaka Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya wote watakaothibitika
kuhusika kuliingizia Taifa hasara na kuwakosesha Watanzania fursa ya
kufaidika na rasilimali za madini.
Hoja
hiyo imetolewa leo Jumatano bungeni baada ya kamati iliyoundwa jana na
Spika Job Ndugai kupata maoni ya namna Bunge linavyoweza kuunga mkono
juhudi binafsi zinazochukuliwa na Rais John Magufuli kukabiliana na
udanganyifu unaofanywa kwenye sekta hiyo.
Kamati
hiyo iliyoongozwa na Mbunge wa Newala Mjini, George Mkuchika baada ya
kukamilisha taratibu zote, imetoa maazimio matatu ambayo yamepitishwa na
Bunge.
"Bunge
linamuunga mkono Rais John Magufuli na lipo tayari kutoa ushirikiano wa
dhati kadri itakavyohitajika kuhakikisha juhudi hizi hazipotei bure na
sekta ya madini inachangia maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla,"
amesema Mkuchika.
Kukubaliana
na kinachofanywa na Rais Magufuli maazimio matatu yametolewa ambayo ni
kumpongeza na kuunga mkono kwa hatua anazochukua, kumhakikishia
ushirikiano wakati wowote atakapohitaji na kushauri kuchukuliwa kwa
hatua kali za kisheria kwa watakaobainika kushiriki kulitia taifa hasara
kutokana na kuidhinisha mikataba mibovu na wizi uliofanywa.
0 comments:
Chapisha Maoni