BODI ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) imemsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Dk James Mataragio.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya shirika hilo na wadau mbalimbali wa masuala ya mafuta na gesi, zimeeleza kuwa kusimamishwa kazi kunatokana na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) ya mwaka jana iliyoeleza kuwa, TPDC ilikiuka taratibu za manunuzi ya umma kwa kuipa upendeleo kampuni ya Marekani kutafiti mafuta na gesi katika maeneo ya kaskazini na magharibi mwa Ziwa Tanganyika, Songosongo, Mandawa na Eyasi.
“Shirika kwa sasa si salama, kwani mkurugenzi amepewa barua kutoka kwa mwenyekiti wa bodi kusimamishwa kazi kuanzia jana (Jumatano) kutokana na ripoti ya ukaguzi,” alisema mmoja wa watoa taarifa.
Hata hivyo, mpaka jana jioni hakukuwa na taarifa rasmi kuhusu kusimamishwa kazi kwa mkurugenzi huyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa alipoulizwa kuhusu hatua hiyo, alisema anafahamu suala la kusimamishwa kazi kwa Dk Mataragio, lakini akaongeza kuwa, maelezo zaidi kuhusu maamuzi hayo anayo Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Profesa Sufian Bukurura.
Hata hivyo, Mwenyekiti huyo alipotafutwa kwa simu kutoa taarifa rasmi za kusimamishwa kazi kwa mkurugenzi huyo, hakupatikana kwani mara zote simu yake ilisema inatumika.
Dk. James P. Mataragio ni Mtanzania ambaye alishika nafasi hii baada ya kuteuliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete toka 15 Desemba 2014.Kabla ya kipindi hicho aliishi na kufanya kazi nchini Marekani akiwa Senior Geoscientist wa Kampuni ya Bell Geospace, Houston, Marekani. Wasifu wake ni kama ifuatavyo:-
ELIMU:-
• Masters in Business Development (MBA), Chuo Kikuu cha Charlotte, North Caroline, Marekani (2008)
• PhD (Geochemistry, Mineralogy, Structural Geology and Petroleum Geology), Chuo Kikuu cha Missouri – Rolla, Missouri, Marekani (2005)
• MSc (Geochemistry and Petrology), Chuo Kikuu cha Okinawa, Japan (1997)
• BSc(Hons) (Geology), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 1994

UZOEFU WA KAZI:-
2014- 2016 - Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la TPDC
2014- 2016 - Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la TPDC
•Mwaka 2004 – 2014, Senior Geoscientist, Bell Geospace Inc, Houston, Texas, USA
• 2001 – 2004, Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Missouri, wakati akisoma Shahada ya Uzamivu
• 2000 – 2001, Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
• 1999 – 2000, Meneja Mradi, Anglo Gold (Buzwagi)
• 1994 – 1999 -, Exploration Geologist, Anglo America Corporation.
Miongoni mwa makampuni makubwa ya kimataifa ya mafuta na gesi aliyofanya nayo kazi kwa niaba ya mwajiri wake Bell Geospace ni pamoja na Petrobras (Brazil); BP; Anadarko; Tullow; Pemex (Mexico); ANP (Brazil), Ecopetrol (Colombia); Petronas, (Malaysia) na Vale Rio Doce.

Aidha, Dk. James P. Mataragio ni mmoja wa wataalam wa sekta ya madini, mafuta na gesi asilia waishio Marekani (Diaspora) ambao walijitolea kuishauri Serikali kuhusu sekta hiyo bila malipo.
Kwa kuzingatia elimu yake, uzoefu wake na uzalendo wake,lakini fyekeo limempitia.