Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ameondolewa mamlaka ya kutoa adhabu isiyokatiwa rufaa kwa mshtakiwa anayekiri makosa ya kimtandao.
Uamuzi
huo umetolewa na Mahakama Kuu,umeipa Serikali miezi 12 kukifanyia
marekebisho kifungu cha 50 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao
kilichobatilishwa.
Hata
hivyo, mahakama hiyo imehalalisha vifungu vingine vyote vya sheria
hiyo, ambavyo pia vimekuwa vikilalamikiwa na wadau wa matumizi ya
mitandao na teknolojia ya habari.
Uamuzi
huo umetokana na kesi ya kikatiba, iliyofunguliwa na Mtandao wa
Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki
za Binadamu (LHRC)na mashirika mengine.
Katika
hukumu iliyotolewa na majaji Profesa John Ruhangisa, Winfrida Korosso
na Lugano Mwandambo, Mahakama ilibatilisha Kifungu cha 50 cha sheria
hiyo, lakini ikaridhia vingine kuwa ni halali.