Baadhi ya mashabiki na wanachama wa Yanga walivamia ofisi
za Makao Makuu ya klabu jana usiku wakimtaka Katibu Mkuu, Charles
Boniface Mkwasa.
Mashabiki walijiitokeza Makao Makuu ya klabu wakimtamka
Mkwasa awape ufafanuzi kuhusiana na kuondoka kwa Kocha George Lwandamina
ambaye amerejea kwa Zambia kujiunga na timu yake ya zamani, Zesco
United.
Baada ya kuwasili ofisini hapo, wengi wameonekana
wakimtupia lawama Mkwasa, wakisema kuwa yeye ndiye chanzo cha kuondoka
kwa Lwandamina kimyakimya.
Taarifa zilizoripotiwa baada ya kuondoka kwa Lwandamina,
zinaeleza kuwa Mkwasa na Kocha huyo hawakuwa na maelewano mazuri haswa
katika masuala mazima ya utendaji.
Mbali na utendaji, inaelezwa pia Mkwasa ana mpango wa kuachana na wadhifa wa Ukatibu Mkuu ili kuchukua nafasi ya Lwandamina.

0 comments:
Chapisha Maoni