Uongozi
wa gazeti la MAWIO umeapa kwenda mahakamani kupinga uamuzi wa serikali
kulifungia gazeti hilo kutochapishwa kwa kipindi cha miezi 24.
Uamuzi
wa kulifungia gazeti hilo ulitangazwa na serikali kupiti Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambapo sababu iliyotajwa ni gazeti
hilo kukiuka maagizo ya serikali ya kutowahusisha marais wastaafu Mzee
Mkapa na Dkt Kikwete katika ripoti za uchunguzi wa mchanga wa madini.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Victoria Media Services Ltd ambaye pia ni Mhariri
Mtendaji wa gazeti la MAWIO, Simon Martha Mkina, aliliambia The Citizen
kuwa, amuzi huo si wa haki na utapingwa mahakamani.
“Bodi
itakutakana kujadili uamuzi huo kama jambo la dharura, lakini
tunachoweza kukwambia kwa sasa, tutakwenda mahakamani,” alisema Mkina.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Waziri Dkt Mwakyembe iliyotolewa na Idara ya
Habari (MAELEZO), Waziri alinukuliwa akisema, “Sina budi kulifungia
gazeti lako, na kukutaka usitishe kuchapisha nakala ngumu au ya
mtandaoni katika kipindi cha muda wa miezi ishirini na nne (24) tangu
tarehe ya barua hii, kwa mamlaka niliyopewa chini ya Sheria ya Huduma za
Habari Na. 12 ya mwaka 2016 kifungu cha 59.”
Gazeti
hilo liliandika habari iliyokuwa na ujumbe wa jumla kuwa, marais hao
wamelisababishia taifa hasara kubwa sana kutokana na usafirishaji wa
mchanga nje ya nchi kwa kipindi cha miaka 19.
Kwa
mujibu wa mamlaka iliyonayo kupitia Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976
sura ya 229 kifungu cha 25(1), Januari 15, 2016 Serikali ilitangaza
kulifungia kwa muda wote gazeti la MAWIO lakini baada ya mwaka mmoja wa
kukaa kifungoni lilirejea mtaani baada ya kushinda rufaa mahakamani.
0 comments:
Chapisha Maoni