Upelelezi
dhidi ya kesi ya kumshambulia askari polisi inayomkabili aliyekuwa
Naibu Waziri wa fedha na mbunge wa Mkuranga, Adam Kigoma Malima
umekamilika.
Mwendesha
Mashtaka, Wakili wa Serikali Esta Martin amemueleza Hakimu Mkazi,
Godfrey Mwambapa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa kesi hiyo jana
ilikuja kwa kutajwa.
"Mheshimiwa,
kesi hii Leo(jana) imekuja kwa kutajwa lakini upelelezi umekamilika, tu
naomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuja kuwasomea washtakiwa maelezo
ya awali (PH), alidai Martin.
Hakimu
Mwambapa aliiahirisha kesi hiyo kwa niaba ya Hakimu Mkazi Respecious
Mwijage ambaye ndio amepangwa kusikiliza kesi hiyo kwa kuwa anaudhuru.
"Hakimu
aliyepangwa kusikiliza kesi hii anaudhuru, naiahirisha hadi Julai 10
itakapokuja kwa ajili ya kusomewa PH mbele ya Hakimu husika", alisema
Hakimu Mwambapa
Malima anashtakiwa pamoja na dereva wake Ramadhani Mohamed Kigwande anayekabiliwa na tuhuma za kujeruhi.
Katika
hati ya mashtaka ilidaiwa kuwa, Mei 15 mwaka huu huko Masaki katika
wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam mshtakiwa Malima alimzuia afisa
wa polisi mwenye namba H.7818 PC Abdul kufanya kazi yake ya kumkamata
dereva wake Kigwande aliyekuwa amefanya kosa la kumjeruhi Joseph Mwita
ambaye ni afisa operation wa Priscane Business Enterprises.
Ilidaiwa
kuwa, siku na mahali hapo, mshtakiwa Kigwande kwa nia ya kukataa
kukamatwa, alimjeruhi afisa operation hiyo(Joseph Mwita) ambaye alikuwa
anakamatwa kwa kosa la kupaki gari vibaya na kumsababishia Mwita
Majeraha Mwilini.
Watuhumiwa wote wako nje kwa dhamana na upelelezi bado haujakamilika.
Aidha,
Wakili wa utetezi Peter Kibatala alishindwa kuwasilisha pingamizi la
awali juu ya mapungufu ya kisheria yaliyopo kwenye shtaka la shambulio
linalomkabili Malima Peke yake kwa kuwa Hakimu husika anaudhuru.
Mapema
mwezi huu, Kibatala aliitaarifu Mahakama kuwa jana angewasilisha
pingamizi kuwa shtaka linalomkabili Malima, maelezo ya kosa na tuhuma
hazifanani.
0 comments:
Chapisha Maoni