Msafara
wa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa ukiwa na magari manne
ukisindikizwa na magari mawili ya polisi umewasili makao makuu ya
polisi.
Jana Lowassa alipewa taarifa ya kwenda kuhojiwa kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).
Mapema
leo, Jumanne asubuhi polisi wameimarisha ulinzi katika barabara zote
zinazoingia Makao Makuu ya Jeshi la Polisi yaliyopo Mtaa wa Ohio.
Polisi
wakiwa na silaha wameegesha magari yao kwenye kila barabara inayoingia
makao makuu ya jeshi hilo, huku wengine wakizunguka zunguka maeneo ya
jirani.
Wananchi
wanaruhusiwa kupita lakini walio kwenye vikundi wanasimamishwa na
kuhojiwa, huku wengine wakizuiwa kabisa kukatiza eneo hilo.
0 comments:
Chapisha Maoni