Mwanafunzi
aliyefukuzwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Alphonce Lusako,
amewasilisha maombi Mahakama Kuu chini ya hati ya dharura, aruhusiwe
kukishtaki chuo hicho kwa kumkatisha masomo.
Mwanafunzi
huyo aliyekuwa akisoma shahada ya kwanza ya sheria alifukuzwa baada ya
kufutiwa usajili Januari 26, pamoja na mambo mengine akidaiwa kusajiliwa
kwa makosa kwasababu aliwahi kufukuzwa chuoni hapo.
Lusako
anayewakilishwa na Wakili Jebra Kambole anaiomba Mahakama impe kibali
cha kuishtaki UDSM na itoe amri ya kuzuia uamuzi wa kumfutia usajili.
Maombi hayo yamepangwa kusikilizwa Mei 23 na Jaji Pellagia Khaday.
Lusako alijiunga na UDSM kwa mara ya kwanza mwaka 2009 akiwa amedahiliwa kusoma Shahada ya Biashara katika Uhasibu.
Hii
ni mara ya pili kwa Lusako kufukuzwa chuoni hapo, mara ya kwanza ni
Desemba 13, 2011, pamoja na wenzake kadhaa, akiwa mwaka wa tatu
walifukuzwa na kufutwa katika mfumo wa elimu nchini wakidaiwa kuratibu
mgomo wa wanafunzi UDSM.
Hata
hivyo, anadaiwa alikuwa akipinga ufisadi katika Tume ya Vyuo Vikuu
(TCU) kwa kusajili wanafunzi hewa na katika Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi
wa Elimu ya Juu (HESLB).
Baada ya kukaa uraiani kwa muda mrefu, aliamua kuomba usajili, TCU ilimsajili na kumpanga UDSM kusoma kozi ya sheria.
Baada
ya kusoma muhula mmoja, alipewa barua ya kufutiwa usajili ikieleza
alisajiliwa kimakosa chuoni hapo kwa kuwa tayari alishawahi kufutiwa
usajili.
0 comments:
Chapisha Maoni