Mamlaka
ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imeyafunga nusu ya machinjio ya
ng’ombe, kuku na nguruwe katika Manispaa za Temeke, Ilala, Ubungo na
Kinondoni baada ya kufanya ukaguzi.
Mkurugenzi
wa TFDA, Hiiti Sillo alisema kuwa ukaguzi huo uliofanyika katika
machinjio 55 kwa kushirikiana na Bodi ya Nyama, Wizara ya Kilimo, Mifugo
na Uvuvi na Maofisa Afya na mifugo, umebaini 26 yamekiuka kanuni na
sheria, hivyo kuyafunga.
“Lengo
la ukaguzi ilikuwa kuangalia utekelezaji wa Sheria ya Chakula, Dawa na
Vipodozi Sura ya 219, hususan kukagua majengo, miundombinu, mfumo wa
uchinjaji na uendeshaji wa machinjio kama unazingatia kanuni”, alisema
Sillo.
Alitaja
sababu za kufungwa kwa machinjio hayo kuwa ni kutokuwa na majengo ya
kudumu miundombinu isiyofaa, uchinjaji usiozingatia kanuni, ukiukwaji wa
sheria za kuendeshea machinjio na uchafu ndani na nje ya machinjio.
Meneja
wa TFDA Kanda ya Mashariki, Emmanuel Alphonce, alisema barua
zimeandaliwa ili kupelekwa kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwaajili
ya machinjio ya Vingunguti na uongozi wa Mazizini, baada ya TFDA kutoa
siku saba kwa uongozi wa machinjio hizo, kufanya marekebisho ya upungufu
uliobainika ambao ni uuzwaji wa nyama ndani ya machinjio na uingiaji wa
watu wasiohusika.
0 comments:
Chapisha Maoni