Korea
Kaskazini imedai kwamba kombora la masafa marefu lililofanyiwa
majaribio siku ya Jumapili ni kombora jipya linaloweza kubeba kichwa cha
nyuklia.
Kombora
hilo lililorushwa lilienda angani urefu wa kilomita 2,000 na kusafiri
kilomita 700 kabla ya kuanguka katika bahari Magharibi mwa Japan.
Majaribio
ya mara kwa mara ya makombora ya masafa marefu yanayofanywa na taifa
hilo yanakiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa na yamesababisha wasiwasi
miongoni mwa jamii ya kimataifa pamoja na Marekani.
Marekani na Japan zimetaka kufanyika kwa mkutano wa dharura katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne.
Shirika
la habari la Korea Kaskazini KCNA, limesema kwamba jaribio la kombora
jipya la masafa marefu la Hwasong 12, lililenga kuonyesha kwamba kombora
hilo jipya lina uwezo wa kubeba kichwa cha Nyuklia.
0 comments:
Chapisha Maoni