Askofu
wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amewaonya baadhi ya watu
wanaoiongelea vibaya nchi akiwataka waache mara moja kwa kuwa
wanachochea uvunjifu wa amani.
Askofu Gwajima amesema kinachotakiwa watu waizungumzie nchi vizuri kwa kuwa amani itakuwepo na uchumi wa nchi utaendelea kukua.
"Namkemea yule mtu ambaye anaiongelea vibaya nchi yetu huwezi ukawa unatoa kinywa kinachoashiria uvunjifu wa amani,"
"Huwezi
kila siku unalaani kwa kuiongelea vibaya nchi yetu lazima nikemee ili
nchi yetu iweze kuendelea kuwa na amani,"amesema Gwajima katika mahibiri
kanisani kwake leo.
0 comments:
Chapisha Maoni