![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh7CTDMGI_NgEuGyh0zf2uatojryocn6roQlzARwW2xTSZvKez4L7ucB9ElDwuYUqbylbnf3RS3Oo8EEaVNTJ8n44j1Hcs8qX-tC14saBxr-BZ3iuiyWmPRLLOiRt_YK3A7xSVugu_5bYQH/s640/1.jpg)
Kaimu
katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano)
Dkt. Injinia Maria Sasabo akiishukuru kampuni ya Bharti Airtel kwa
kuuza hisa 35 ili Serikali iweze kuendeleza mikakati yake ya kuimarisha
TTCL. Prof. Tolly Mbwete, Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL (wa kwanza kulia)
na Bwana Lawrence Mafuru, Msajili wa Hazina (wa kwanza kushoto)
wakifuatilia tukio hilo.
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina
imefanya makabidhiano ya hati ya kuiwezesha Serikali Kumiliki Hisa za
Kampuni ya TTCL kwa asilimia 100 ambapo hisa ailimia 35 zilikuwa
zinamilikiwa na Kampuni ya Bharti Airtel.
Utiaji
saini huo umefanyika baina ya Bwana Larewnce Mafuru, Msajili wa Hazina
na Bwana Christian Manuel De Faria, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel,
Afrika.
Makabidhiano
hayo yamefanyika leo Dar es Salaam tarehe 23 Juni, 2016 kwenye Ofisi za
Makao Makuu ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na kushuhudiwa na Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
anayeshughulikia Sekta ya Mawasiliano Dkt. Injinia Maria Sasabo, Prof.
Tolly Mbwete, Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL na Dkt. Kamugisha Kazaura,
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL.
Kabla ya tukio hilo la leo, Serikali kupitia TTCL ilikuwa ina miliki hisa hizo kwa alisimia 65 na Bharti Airtel kwa asilimia 35.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano