Klabu
ya Yanga ilianza vyema mchezo ndani ya dakika za mwanzo kabisa na
kupelekea mchezaji Obrey Chirwa mwenye jezi namba 7 mgongoni kufanyiwa
madhambi ndani ya kumi na nane na mchezaji wa Simba Novat Lufunga na
kupelekea Yanga kupata penati ndani ya ya dakika 4 za mchezo na kupigwa vyema na mchezaji Simon Msuva wa Yanga.
Yanga
iliendelea kuongoza kwa bao hilo la kwanza huku wakiwa na moto wa
kutafuta goli la pili, katika dakika ya 23 Yanga walipata kona ya kwanza
ambayo ilipigwa na mchezaji Haruna Niyonzima lakini kipa wa Simba
aliweza kuicheza vyema na kuondoa hatari ya Yanga kupata goli la pili
ndani ya dakika za mwanzo mwanzo.
Kocha
wa Simba Omug alipoona kikosi chake hakina mwenendo mzuri ndani ya
dakika 27 alimtoa Luizio na kumuingiza Said Ndemla ambapo hapo kidogo
mchezo kwa upande wa Simba ulibadilika na kuanza kufanya mashambulizi,
huku wakijaribu
Ndani
ya dakika 32 Goli kipa wa Yanga Deogratius Munishi alidaka mpira na
kukaa nao kwa muda na kupeleka faulo ambayo ilipigwa na Said Ndemla wa
Simba lakini Ndemla alikosa na kupoteza nafasi ya kusawazisha goli la
kwanza.
Yanga
iliendelea kufanya vyema na kujaribu mara kadhaa katika lango la Simba
bila mafanikio, ndani ya dakika 43 Simba ilibahatika kupata faulo
nyingine tena ambayo ilipigwa na mchezaji Ajib lakini mpira huo
ulikwenda nje.
Mchezo
uliendelea kwa kasi na mashambulio kwa timu zote mbili, na ilipofika
dakika ya 47 mchezaji wa Yanga Thabani Kamusoko alitoka nje baada ya
kupata majeraha na kuingia Said Juma Makapu.
Mpaka
muda wa mapumziko Yanga ilikuwa ikiongoza kwa bao moja dhidi ya Simba
huku ikiwa imetawala mchezo kwa asilimia 51 na Simba ikitawala mchezo
kwa asilimia 41.
Baada
ya kurudi kwa kipindi cha pili timu zote mbili zilikuwa na hamasa ya
mchezo na ushindi hamasa hizo zilipelekea mchezaji wa Yanga, Endrew
Vicenti alipata kadi ya njano ndani ya dakika 56 mchezaji wa Simba
alipigwa kadi nyekundu na kutoka nje ya uwanja na kuwaacha Simba wakiwa
pungufu uwanjani.
Katika
kipindi cha pili baada ya kuingia mchezaji Kichuya Simba ilibadilika na
kuanza kufanya mashambulizi ya mara kwa mara na kuonyesha uwezo katika
kucheza mpira jambo lililopelekea mchezaji Mavugo wa Simba ndani ya
dakika 66 kupata goli la kwanza kwa Simba na kuweza kusawazisha na kuwa
bao moja kwa moja.
Mpka
dakika ya themanini ya mchezo Simba kupitia kwa mchezaji wake Shiza
Ramadhan Kichuya aliiandikia Simba goli la pili dhidi ya Yanga huku timu
hiyo ikiwa pungufu uwanjani.