Mamlaka
ya Chakula na Dawa (TFDA) imeyafungia machinjio 26 kati ya 55 jijini
hapa katika Manispaa za Ubungo, Kinondoni, Ilala na Temeke.
Mkurugenzi
Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo amesema hayo leo akizungumza na waandishi wa
habari kuwa ukaguzi ulianza Mei 2-12 na kuwahusisha wadau wote muhimu
wakiwemo Bodi ya Nyama na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
"Lengo
la ukaguzi huo ulikuwa kuangalia utekelezaji wa Sheria ya Chakula, Dawa
ya Vipodozi... Ulifanyika usiku kwa machinjio ya ng'ombe na asubuhi na
mchana kwa machinjio ya kuku na nguruwe," amesema Sillo.
Amesema katika machinjio 26, moja ni ya ng'ombe, 14 nguruwe na 11 ya kuku.
0 comments:
Chapisha Maoni