Katibu
wa Chadema, Kanda ya Iringa Mjini, Suzana Mgonokulima, ametangaza
kumvua uanachama aliyekuwa diwani wa chama hicho, Kata ya Gangilonga,
Dady Igogo. Igogo pia alikuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa.
Katika
taarifa iliyotolewa leo Aprili 28, imeelezwa kuwa Igogo amevuliwa
uanachama kwa kuwa alikisaliti chama kwa kujivua nafasi ya unaibu meya
na baadaye udiwani.
“Ndugu
Igogo kwa muda mrefu amekuwa na mwenendo usioendana na itikadi,
falsafa, madhumuni, kanuni, maadili na sera za chama,” imesema taarifa
hiyo.
Taarifa
hiyo imesema kamati tendaji ya jimbo katika kikao chake cha dharura
kilichoketi Aprili 24 mwaka huu kiliadhimia Igogo avuliwe ujumbe wa
kamati tendaji ya jimbo, kwa kwenda kinyume na katiba ya chama kanuni na
maadili.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Igogo amevuliwa uanachama kuanzia leo Aprili 28 kama ilivyokubaliwa na wajumbe wa kamati.
0 comments:
Chapisha Maoni