Waziri
Mkuu wa Shirikisho la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Ethiopia Mhe.
Hailemariam Dessalegn ameondoka nchini leo kurejea nchini mwake Ethiopia
baada ya kumaliza ziara yake rasmi ya kiserikali hapa nchini
aliyoifanya kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli.
Katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam,
Mhe. Hailemariam Dessalegn ameagwa na mwenyeji wake Mhe. Rais Magufuli
aliyeongozana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Kassim Majaliwa Majaliwa.
Akiwa
nchini Mhe. Hailemariam Dessalegn amefanya mazungumzo na mwenyeji wake
Mhe. Rais Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam, amehudhuria dhifa ya
kitaifa iliyoandaliwa na Mhe. Dkt. Magufuli kwa heshima yake na leo
asubuhi ametembelea bandari ya Dar es Salaam ambapo amesema nchi yake
ipo tayari kuitumia bandari hiyo sambamba na kuanzisha kituo cha huduma
za usafirishaji wa mizigo kwa ndege (Cargo Hub) katika Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere kupitia shirika lake la ndege la Ethiopia
Airline.
Emmanuel Buhohela
Kaimu Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi
Dar es Salaam
01 Aprili, 2017