Serikali
imesema jumla ya walimu 3,081 wakiwemo walimu 7 wa shule ya Sekondari
Omumwani Kagera, wameajiriwa, hivyo bado kuna nafasi ya walimu 1.048
kati ya nafasi 4,129 za walimu wa Sayansi na Hisabati zilizotolewa
kibali cha ajira.
Taarifa
hiyo imetolewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene alipokuwa akizungumza
na Waandishi Habari,ofsini kwake ambapo amewataka walimu wote
walioajiriwa wanatakiwa kuripoti katika vituo vyao vya kazi kuanzia
tarehe 18 hadi 25 mwezi huu.
Amesema
walimu walioajiriwa wamepangwa moja kwa moja na TAMISEMI katika
halmashauri zote nchini ambazo zina upugufu wa walimu wa Sayansi na
Hisabati.
Simbachawene amesema kati ya walimu hao walioajairiwa walimu 1,537 ni wa Shahada na walimu 1,544 ni wa Stashahada.
“Sehemu
kubwa ya walimu wa Shahada wamepangwa kwenye shule za kidato cha tano
na sita na wachache kwenye shule za kidato cha kwanza hadi cha nne’’
alisema.
Simbachawene
amekiri kuwa kuna upungufu wa walimu 26,026 wa masomo Sayansi na
Hisabati katika shule mbalimbali za sekondari nchini.
“Moja
ya changamoto kubwa ambazo zinaikabili sekta ndogo ya elimu ya
sekondari ni upungufu wa walimu wa Sayansi na Hisabati upungufu uliopo
katika shule 3,602 ni 26,026 sawa na asilimia 60.14 ya walimu 43,248
wanaohitajika” amesema Simbachawene
Amesema walimu wanaohitajika kwa masomo hayo ni walimu 43,248 lakini waliopo kwa sasa ni 17,252 pekee.
Amesema
kwa sasa serikali ina shule za sekondari 3,602 na kati ya hizo shule
333 ni za kidato cha tano na sita huku zingine 54 za kidato cha tano
zimeanzishwa .
Aidha
amesema shule hizo za sekondari kwa upande wa masomo ya Sanaa ina ziada
ya walimu 7,463 ambapo waliopo ni walimu 63,240 na wanaohitajika ni
walimu 55,777.
“Kutokana
na ziada hiyo ya walimu wa Sanaa serikali imeanza kuchukua hatua
yawahamisha walimu hao katika shule za msingi ili kuziba upungufu wa
walimu katika shule hizo’’ alisema.