ya kutumbuliwa na Rais Magufuli juzi, leo akiwa chini ya ulinzi wa Polisi wakitoka ofisini kukagua. Account feki ya maafa Kagera."
Ujanja ujanja hakuna.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, kwa vyombo vya habari jana ilieleza hayo.
Msigwa asema pia kuwa kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, pamoja na kutengua uteuzi huo, Rais Magufuli ameagiza vyombo vya dola vichukue hatua dhidi ya wote waliohusika katika njama za kufungua akaunti hiyo.
Taarifa hiyo ya Ofisi ya Waziri Mkuu ilieleza kuwa Majaliwa amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Swai kutokana na kuhusika katika njama hizo.
Hata hivyo, Majaliwa ametoa mwito kwa wananchi na taasisi mbalimbali, kuendelea kuchangia misaada kwa ajili ya walioathirika kwa kutumia akaunti rasmi ya “Kamati Maafa Kagera” ambayo imetangazwa na Serikali.