ILIPOISHIA
Makachero
wanao uongoza msafara huo wakashuka kwenye magari yao kila mmoja akiwa
na bastola iliyo jaa risasi mkononi mwake. Wakatembea kwa tahafhari
kubwa wakijaribu kuchunguza kila sehemu ya msitu huo kwa umakini wa hali
ya juu. Umakini wao ulizidi kuongezeka kwani wana kiongozi wao mkubwa
wa nchi. Wakafika hadi eneo la handaki. Makachero wawili wakaingia ndani
ya handaki hilo. Gafla milio mingi ya risasi ikasikika ndani ya handaki
hilo jambo lililo wachanganya raisi na watu wake walio baki nje ya
handaki.
ENDELEA
Milio hiyo ya risasi ikawafanya makachero wengine kumzunguka raisi
Praygod Makuya kuzuia hata kama kuna tatizo baya litatokea waweze
kumlinda. Ikawalazimu makachero wawili kuingia katika handaki bastola
zao zikiwa mikononi mwao. Cha kushangaza wakawakuta wezao wakiwa
wamesimaa huku wanatetemeka mithili ya watu walio mwagiwa maji ya
baridi na kusimamishwa kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro.
Wakajaribu
kuwauliza kwa ishara ni kitu gani kimepelekea hadi wakawa wanafyatua
risasi ovyo ovyo. Ila hakuna aliye weza kutoa jibu kati yao zaidi ya wao
kuendelea kutetemeka. Ikawalazimu wezao hao wawili kuanza kutembea
taratibu ndani ya handaki hilo kuchunguza ni nini ambacho kimetokea.
Wakaingia
kwenye moja ya chumba ambapo cha kwanza kukutana nacho chini ni damu
nyingi za mwanadamu. Katika kupitisha pitisha macho yao huku na huku.
Wakamkuta mke wa raisi akiwa amelala juu ya kitanda huku damu nyingi
zikiwa zinamwagika mwilini mwake, akikaribia kuiaga dunia.
***
Kitu kisicho onekana kikazidi kuwateketeza makachero walio mshambulia Priscar hadi wote wakafa.
Katika
hali ya kumshangaza Priscar akajikuta akivutwa nje ya gari na kulazwa
pembeni pasipo kumuona mtu anaye mfanyia mambo yote hayo. Jeraha la
risasi iliyo mpiga ndani ya dakika moja likawa limekauka na mwili wake
ukarudi katika hali yake ya kawaida.
“Wewe ni nani unaye nifanyia haya yote”
Ilimbidi
Priscar kuuliza kwani hisia za kusnikwa na mtu huyo asiye oenekana
kwenye mwili wake mara kadhaa, anazihisi ila tatizo ni mboni zake za
macho haziwezi kumuona mtu huyo.
Hakuna
ambacho aliweza kuambulia kujibiwa. Gari lake ambalo limeingia kwa
nyuma ndani ya mtaro akashangaa likisitolewa taratibu na kusimamishwa
barabarani. Kisha akajikuta akishikwa mkono wa kulia akikokotwa hadi
kwenye mlango wa kuingilia ndani ya gari hilo. Mlango ukafunguliwa bila
hata ya kupenda akajikuta akinyanyuliwa na kuingizwa kwenye gari na
kukalishwa kwenye siti ya dereva.
Akafungwa
mkanda, gari ikawashwa na mikono yake ikashikishwa kwenye mskani wa
gari hiyo na mlango ukafungwa. Ikiashiria aondoke katika eneo hilo
haraka iwezekanavyo kwani kuna gari baadhi za polisi zinakuja kuwapa
nguvu makachero wanao pambana na mtu aliye hitaji kuuvamia msafara wa
raisi.
***
Dokta
akamuachia simu Shamsa kisha yeye akazidi kusonga mbele. Kulifwata gari
lililo kosa kosa kuwagonga. Shamsa kabla hajafika hatua nyingi simu
hiyo ikaita kuangalia vizuri akakuta ni jina la baba yake, hakuona haja
ya kuelekea anapo kwenda dokta wake. Akaipokea na kuiweka sikioni mwake.
“Baba habari”
“Ohoo Salama binti yangu, mumefika salama”
“Ndio baba hapa tumefika hospitalini”
“Mbona unazungumza kwa furaha sana?”
“Hpana baba kidogo nimebadilisha mazingira, kidogo ninafurahi sana”
Shamsa
akiendelea kuzungumza na simu tayari dokta wale alisha fika kwenye
gari na kukutana na binti anaye mfahamu akitokea ndani ya gari hilo huku
akimwagikwa na machozi.
“Sa Yoo unatatizo gani?”
Daktari alimuuliza huku hasira yake ikiwa imebubujika kifuani mwake mithili ya barafu la maji liwekwapo juani
“Bibi yangu hali yake ni mbaya”
Dokta
baada ya kusikia hiyo na kutokana anamfahamu vizuri binti huyo pamoja
na bibi yake ambaye pia alisha wahi kumuhudumia katika maswala ya
saikolojia, hakuwa na budi zaidi ya kuondoka na Sa Yoo wakielekea ndani.
Wakaungana na Shamsa kuingia ndani ya hospoitali hiyo pasipo Eddy
kumjua binti wa tatu anaye ingia na kina Sa Yoo ni nani, kwani binti
huyo ameziachia nywele zake ndefu kwa nyuma nakuizuia sura yake kuweza
kuonekana vizuri kwa mbele
Kutokana
na uhalifu alio ufanya Eddy, ikamuwia ugumu kushuka ndani ya gari
kuhofia kuingia mikononi mwa polisi, moja ni lazima astakiwe kwa kusa la
kuwapiga polisi, mbili ni lazima atakabidhiwa katika ubalozi wa
Tanzania aweze kurudishwa Tanzania, jambo ambalo hakuhitaji kuweza
kulisikia kwa wakati huo.
Sa
Yoo na daktari wakakimbilia kwenye chumba cha wagonjwa mahututi huku
wakimuacha Shamsa akiwa amekaa sehemu maalumu ya mapokezi akimsubiria
mwenyeji wake afike. Shamsa akaitumia nafasi hiyo kuweza kumfikiria ni
wapi ambapo anaweza kumpata Eddy.
Mwanaume
anaye muheshimu kama baba yake, wazo la kurudi kwenye familia ya
magaidi wa Al-Shabab likaanza kumpotea taratibu kichwani mwake, akaanza
kufikiria kuungana tena na Eddy ambaye aliamini kwamba amekufa na hilo
ndio jambo ambalo lilimfanya akubali kurudi katika familia ya Al-Shabab
watu walio muulia wazazi wake baba na mama akiwa mdogo kisha
akachukuliwa mateka na kuwa miongoni mwa askari wakikosi hicho akiwa
mdogo sana.
“Nilazima niwaue Al-Shabab wote”
Shamsa
alizungumza huku picha ya askari wa kikosi hicho ikiwajia jia kichwani
mwake. Hasira dhidi ya kikosi hicho ikazidi kumpanda moyoni mwake hadi
mwili mzima ukaanza kumtetemeka.
Kwa
kupitia kioo cha pembeni cha gari alilomo Eddy, akaona gari mbili za
polisi zikija katia maeneo ya maegesho ya hospitalini hapo. Wasiwasi
mwingi ukazidi kumpanda, akataka kushuka na kukimbia akaoona itakuwa ni
hatari sana kwake na itakuwa ni rahisi kwa yeye kuweza kukamatwa na
askari hao. Gari hizo zikazidi kulisogelea gari ambalo Eddy yupo, kwa
haraka ikamlazimu kuweza kuinama ndani gari hilo ili asiweze kuonekana.
Gari
hizo za polisi zikasimama karibu kabisa na gari alilopo. Wakashuka
askari wanne walio valia nguo nyeusi huku viunoni mwao wakiwa
wamening’iniza pingu pamoja na kuchomeka bastola zao zilizomo kwenye
vifuko maalumu vya kuchomekea bastola.
Askari hao wakatizama tizama kila sehemu ya maegesho ya magari hayo
wakionekana kwamba kuna gari wanaitafuta, mmoja wao akaanza kupiga hatua
za kulifwata gari hilo taratibu huku akijaribu kutazama namba ya
usajili ya gari hilo kwani ni gari lililo mbebea muhalifu anayetafutwa
ndani ya Japan nzima.
***
Miliyo ya risasi ilipo kata ndani ya handaki makachero wote walio nje
ya handaki wakiongozwa na raisi Praygod wakaingia ndani huku wakionekana
kuwa na shauku kubwa ya kujua ni kitu gani kinacho endelea ndani ya
handaki. Wakawakuta makachero wa kwanza wakiwa hai huku wamesimama, hata
kabla hawajawauliza wakawaona makachero wengine wakitoka ndani ya
chumba kimoja huku wakiwa wamembeba Rahab anaye endelea kuvujwa na damu
nyingi.
Ikabaki nusu Raisi Praygod kuchanganyikiwa baada ya kumuona Rahab akiwa katika hali hiyo.
“Ah…aaa aahme faafaanyaa nini mke wangu”
Raisi
Praygod aliuliza huku mwili ukimtetemeka, makachero walio tangulia
kuingia ndani ya handaki hilo wakakosa jibu la kuzungumza na fika
wanatambu kwamba wao ndio wameusika katika kumpiga risasi Rahab baada ya
Rahab kuanza kufanya jaribio la kuwashambulia makachero hao ila
akashindwa na kujikuta akipigwa risasi kadhaa zilizo mfanya kuingia
ndani ya chumba huku hali yake ikiwa mbaya sana.
Kutokana
hapakuwa na jibu kwa makachero hao, raisi Praygod akatoa amri ya mke
wake awaishwe mara moja kwenye gari wampeleke hospitali.
Safari
ya kurudi jijini Dar es Salaam ikaanza huku gari hizo zikiendeshwa kwa
mwendo kasi. Ndani ya dakika arobaini na tano wakawa wameingia ndani ya
hospitali ya taifa muhimbili huku hali ya raabu kizidi kuwa mbaya kila
jinsi dakika zilivyo zidi kwenda.
Madaktari
wakaanza kazi ya kumuhudumia mke wa raisi, raisi Praygod akashindwa
kuyazuai machozi yake.kumwagika. Hakujali kama ni kiongozi wa nchi
alicho kihitaji kwa wakati huo ni kusikia mke wake anaendelea vizuri.
Madaktari ndani ya chumba cha upasuaji wakafanikiwa kutoa risasi zote sita zilizo ingia ndani ya mwili wa Rahab.
“Dokta…….”
Nesi
mmoja alimuita daktari kiongozi wa opereshini hiyo, macho yao wote
yakatua kwenye mwili wa Rahab, hapakuwa na mtu aliye weza kuamini kitu
walicho kiona, woga kati yao ukazidi kutawala madaktari wote sita pamoja
na nesi mmoja waliomo ndani ya chumba hicho. Vidonda vilivyo kuwa
kwenye mwili wa Rahab vilijiziba na kurudi katika hali ya kawaida.
Kitendo
cha Rahab kuyafumbua macho yake yaliyo mekundu mithili ya damu
kikawafanya madaktari wpte waliomo ndani ya chumba kuanza kukimbilia
mlangoni, kila mmoja akijaribu kuyaokoa maisha yake. Hadi wanafika
mlangoni tayari Rahab alisha simama wima na kuchomo sindano zote za
madripu zilizo kuwa zimechomwa mwilini mwake. Kila walipo jaribu
kuufungua mlango haukufunguka na taa zilizomo ndani ya chumba hicho
zikaanza kufifia na kigiza cha mbali kikaanza kutawala ndani ya chumba.
***
Njia nzima Priscar akajikuta akijiuliza maswali ni kitui gani kilicho weza kutoke katika muda mchache uliopita.
“Au naota?”
Swali
hilo alilipatia jibu akilini mwake kwamba kila kitu kinacho tokea kwa
wakati huo si ndoto bali ni hali alisi inayo jitokeza.
“Madam”
Priscar
aliwaza sehemu alipo mucha Rahab, ikamlazimu kuongeza mwendo kasi wa
gari lake kuelekea nje ya jiji la Dar es Salaam. Hadi anafika katika
maeneo ya hamdaki ikamlazimu kusimaisha gari lake mbali kidogo na sehemu
na lilipo hamdaki, akashuka na kuanza kukimbia kuelekea sehemu ya
handaki, kabla hajalifikia akasikia milio kadhaa ya risasi ikirindima
ndani ya handaki hilo.
Alipo
chunguza vizuri akaziona gari za ikulu zikiwa zimesimama nje ya handaki
hilo, huku Raisi Praygod akiwa wamezungukwa na walinzi wake. Baada ya
milio ya risasi kunyamaza akawashuhudia walinzi hao wakiongozana na
raisi wakiingi ndani ya handaki hilo. Baada ya dakika tano mbeleni
akawaona wakitoka wakiwa wamembeba Rahab akionekana akiwa katika hali
mbaya.
Priscar
akataka kujitokeza ili akasaidiane nao ila akaona itakuwa ni hatari
kwake, akaendelea kujibanza kwenye mti huo hadi wakaondoka kwa kasi
katika eneo hilo.
Kudhibitisha
ni kitu gani kilicho weza kutokea ndani ya handaki hilo, kwa haraka
akakimbia nje ya handaki hilo kutazama ni nini kilicho tokea.
Hakuamini
macho yake baada ya kukuta damu nyingi zikiwa chini ya sakafu zikitokea
katika chumba alipo ingia akazidikuta zikiwa nyingi jkuu ya kitanda.
Jasho likaanza kumtirirka akifikiria ni kitu gani ambacho kimetokea bosi
wake.
Kwa
haraka akatoka ndani ya handaki na kurudi alipo liacha gari lake.
Akaingia ndani ya gari na kuanza kuelekea Dar es Salaam akiamini kwamba
ni lazima Rahab atakuwa amepelekwa kwenye moja ya hospitali iliyopo
jijini Dar es Salaam.
Kwa bahati nzuri akabahatika kuweza kuuona msafara wa raisi kwa mbali,
kwa tahadhari kubwa akaufwatilia hadi katika hospitali ya Muhimbili.
Magari yalipo ingia katika geti kubwa la Muhimbili na yeye
akalisimamisha gari nje na kushuka na kuanza kuelekea katika geti.
Walinzi wa getini wakamzuia asiingie ndani ya geti hilo kutokana ni
majira ya usiku.
Akatoa kitambulisho chake, baada ya askari mmoja kukisoma akamuamuru wezake wamruhusu Priscar kuingia ndani ya hospitali.
“Samahani nesi kuna mgonjwa ameletwa hapa dakika mbili zilizo pita amepelekwa wapi?”
“Aliye letwa wakati huu ni mke wa raisi na amepelekwa chumba cha upasuji”
“Asante”
Shamsa
akaondoka na kuanza kutembea kwa mwendo wa haraka kuelekea kwenye
chumba cha upasuaji, kabla hajafika akawaona baadhi ya makachero wezake
wa ikulu wakiwa nje ya chumba hicho wakiwa wameimarisha ulinzi mkali nje
ya chumba hicho kuku raisi akimwagikwa na machozi.
Katika
hali ya kustaajabisha Priscar akashuhudia damu nyingi zikiruka kwenye
kioo cha dirisha cha chumba hicho pasipo hata walinzi walio kipa mgongo
chumba hicho kushuhudia tukio hilo.
Kwa
haraka akaanza kukimbia kuelekea kwenye chumba hicho, makachero wezake
wanao mfahamu wakabaki wakimshangaa, mmoja wao akataka kumzuia ila
akaambuliwa kusukumwa pembeni hadi raisi aliye kuwa emekaa akanyanyuka
kumshnagaa binti huyo aliye mpa majukumu ya kumlinda mke wake na
akashindwa.
Priscar
bila hata kumjali mtu akaupika teke mlango huo ila haukufunguka, hapo
ndipo watu wote wakatambua kwamba kuna tatizo limetokea ndani ya chumba
hicho baada ya kuziona damu nyingi kwenye kioo cha mlangoni kikiwa
kimetapakaa damu na mbaya zaidi hawasikii kitu chochote mutoka ndani ya
chumba hicho kilicho tengenezwa kwa utaalamu mkubwa wa kuto kutoa sauti
nje wala kuingiza sauti ndani pale mlango unapokuwa umefungwa vizuri.
SORRY MADAM (46) (Destination of my enemies)
Makachero
wote wakisaidiana na Priscar wakaendelea kuusukuma mlango kwa nguvu zao
zote ila hawakupata mafanikio ya kuweza kuufungua mlango huo. Mwanga wa
taa ambao ulikua unafifia ndani ya chumba hicho zikazima na giza
likatawala.
Kila
mtu hususani raisi Pryagod wakawa wamechanganyikiwa hapakuwa na mtu
aliye weza kuelewa ni jambo gani ambalo linaendelea ndani ya chumba
hicho.
“Pigeni risasi mlango hadi uvunjike”
Raisi
Praygod alizungumza huku jasho likimwagika, macho yake yote mawili
yalitwaliwa na rangi ya uwekundu ulio sababishwa na kulia kwa muda
mrefu.
“Muheshimiwa hapa ni hospitali kuna….”
“Pumbavu nimesema vunjeni”
Raisi
Praygod alimfokea mlinzi wake, huku akimpokonya bastola aliyo ishika.
Raisi akaikoki bastola hiyo vizuri kisha akaanza kufyatua risasi kwenye
mlango huo ulio tengenezwa kwa aluminium. Milio ya risasi ikawastua
baadhi ya watu walio kuwa karibu na jengo la upasuaji. Baadhi ya
madaktari na walinzi wa hospitali ikawabidi kukimbila katika jengo hilo
kushuhudia ni jambo gani linalo toklea isitoshe wanafahamu uwepo wa
raisi katika eneo la hospitali.
Wakawakuta
makachero wa raisi wakiushambulia mlango wa chumba cha upasuaji hadi
ukalegea, wakaanza kuupiga mateke ya nguvu hadi ukaanguka chini.
Kwa
giza ambalo limetawala ndani ya chumba hicho hapakuwa na mtu aliye weza
kuona kitu chochote ndani. Kachero mmoja akatoa simu yake mfukoni na
kuwasha tochi, iliyo fanya kila mtu kushuhudia viongo vya binadamu
vilivyo achanishwa na mwili vikiwa vimezagaa zagaa chini, huku damu
nyingi zikiwa zimetapakaa kila kona ya chumba.
***
Askari
akazidi kulisogelea gari ambalo Eddy yupo ndani yake. Katika kutazama
vizuri akaona mtu akiwa ameinama ndani ya gari hilo. Ikamlazimu kuchomoa
bastola yake kiunoni na kuishika vizuri na kuzidi kupiga hatua za
umakini kuelekea kwenye mlango wa gari hilo.
Sa Yoon a daktari wa Shamsa wakaruhusiwa kuingia katika chumba cha
wagonjwa mahututi. Sa Yoo akamkuta bibi yake akiwa amejilaza kitandani
huku manesi wawili wakiwa wamesimama karibu na kitanda chake nyuso zao
zikiwa hazina uchangamfu wowote.
“Bibi…..!!”
Sa
Yoo aliita huku akikaa kwenye kitanda hicho. Kilicho mshangaza katika
siku ya leo ni mashine ya kupumulia iliyo kuwa puani mwa bibi yake leo
haipo. Akaita kwamara ya pili hadi ya tatu machozi yakiendelea
kumwagika. Bibi yake akafumbau macho yake kwa mbali, taratibu bibi huyo
aliye zeeka kutokana na umri mkubwa akaunyanyua mkono wake wa kulia
taratibu na kumshika mjuu kuu wake. Akaachia tabasamu dogo kiasi kisha
akayafumba macho yake moja kwa moja na mauti yakamchukua.
Huzuni
na majonzi ikazidi kutawala kwa kila mtu aliye kuwamo ndani ya chumba
hicho. Sa Yoo, alijikuta akilia kama mtoto mdogo huku akigara gara
chini, kwa msaada wa manesi walifanikiwa kumnyanyua na kumtoa ndani ya
chumba hicho na kumpelekea katika chumba maalumu kwenye hospitali hiyo
ambacho mara nyingi hutumiwa na watu walio fiwa wakiwa katika hospitali
hiyo.
“Daktari vipi mbona umenyongea hivyo?”
“Bibi yake yule binti ameaga dunia”
“Masikini weeee”
Shamsa
alizungumza kwa unyonge ikiashiria hata yeye kifo hicho kimemgusa
kidogo japo hamfahamu marehemu ila kitendo cha kukutana na Sa Yoo muda
mchache ulio pita, moyo wake ulitokea kumepnda binti huyo wa kijapan.
“Nenda kwenye gari yake kula kuna rafiki yake nenda kamuite. Samahani lakini kwa usumbufu”
“Hakuna tatizo daktari”
Shamsa
kwa haraka akaanza kutembea kuelekea nje. Dakika mbili tayari akawa
amefika kwenye gari ya Sa Yoo. Hali aliyo ikuta kwenye gari hiyo kidogo
ikaanza kumpa mashaka kwani mtu aliye ambiwa akamuite hajamkuta. Na kioo
cha pembeni cha gari hiyo kimepasuliwa kwa kupigwa na kitu kizito.
Kila
alipo angaza katika maeneo hayo ya maegesho ya magari hakuweza kuona
dalili yoyote ya mtu aliye ambiwa aende kumuita. Ubaya mtu mwenyewe
hamfahamu ni nani.
Ikamlazimu
Shamsa kurudi ndani ya hospitali akamuelezea hali halisi daktari wake
aliyo ikuta kwenye gari la Sa Yoo. Daktari hakuwa na lolote la kumueleza
Shamsa zaidi ya kunyanyuka katika sehemu waliyo kuwa wamekaa na moja
kwa wakaongozana na Shamsa hadi kwenye chumba alichopo Sa Yoo. Wakamkuta
akiwa amesimama karibu na dirisha macho yake yote yakiwa yatazama nje.
“Sa Yoo”
Daktari
alimuuita, Sa Yoo akageuka taratibu na kuwatazama. Shamsa akapiga hatua
za haraka hadi alipo simama Sa Yoo na kumkumbatia kwa nguvu, jambo
lililo mfanya Sa Yoo kuangua tena kilio kikubwa
***
Manka akiongozana na Fetty, Jaquline, Halima na Anna, wakatua ndani ya
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) majira ya saa tano
usiku, wakitumia shirika la ndege la QATAR. Wakapokelewa na mshauri wa
raisi bwana Mgwira aliye wapeleka moja kwa moja kwenye hoteli ya kitalii
ya iitwayo Bilila Louge.
“Hapa mutakuwa salama zaidi kuliko kwenye mahoteli mengine”
Bwana
Mgira alizungumza huku akitabasamu kwani anatambu ni kazi gani ambayo
masichana hao imewaleta ndani ya Tanzania japo ni wazawa wa Tanzania na
kukulia Tanzania ila matatizo ya hapa na pale yamewafanya kuonekana kama
wageni ndani ya Tanzania.
“Sawa muheshimiwa”
“Hakikiheni hakuna mtu anaye weza kuwatila mashaka, ili kazi iliyo walete isije ikaingia dosari”
“Kwa hilo usijali”
Manka
ndio alikuwa kiongozi wa kumjibu bwana Mgwira. Simu ya bwana Mgwira
ikaita na kuwafanya wote wakae kimya kusikilizia anacho kwenda
kuzungumza.
“Kuna matatizo?”
“Mke wa raisi amefanyeje tena?”
“Mungu wangu!! Ngoja nakuja nachukua ndege ya kukodi”
“Sawa sawa”
Bwana Mgwira akakata simu na kuirudisha kwenye koti la suti.
“Jamani kuna matatizo ya kiofisi yametokea inanilazimu kurudi Dar es Salaam usiku huu huhu”
“Ngoja kwanza mke wa raisi anaitwa nani?”
Fetty alimuuliza bwana Mgwira huku akiwa amemkazia macho.
“Anaitwa Rahab Praygod Makuya”
Fetty
na wezake wakatazamana kila mmoja akawa na shahuku ya kutaka kujua ni
jambo gani limepata rafiki yao waliye potezana naye kwa miaka mingi ya
nyuma.
“Amepatwa na nini?”
Halima aliuliza
“Hata
mimi sijaelezwa kwa kina ila nimeambiwa kwamba ana matatizo makubwa
sana, hapa raisi nasikia amechanganyikiwa ndio maana ninahitajika. Cha
kufanya nitawapa ripoti ya kila jambo ambalo litakuwa linaendelea. Hii
ndio nafasi yetu ya nzuri ya kusimamisha Godwin kama raisi wa hii nchi”
“Sawa”
Bwana Mgrira akatoka na kuwaachia maswali mengiu Fetty na wezake kila mmoja akiwa anahitaji kufahamu kilicho mpata Rahab
***
“Nikiendelea kukaa hapa itakuwa ni matatizo”
Eddy
alijisemea kimya kimya huku akiendelea kuchungulia kwa kuibia katika
kioo cha pembeni cha gari akimtazama askari anaye kuja katika eneo la
mlango wa gari, kwa haraka akaufungua na kumbamiza nao askari huyo,
aliye yumba kidogo. Bila kupoteza muda akatoka ndani ya gari, askari
huyo akarusha teke zitro lililo mpiga Eddy kifuani na kumyumbisha
kidogo, kutokana na mazoezi aliyo nayo, alijizuia kwa asilimia kubwa
asianguke chini kwani hiyo itawapa nafasi askari wengine wanao kuja kwa
kasi katika eneo hilo, kumkamata.
Eddy
akamtazama askari huyo aliye amua kuupanga mkono kupigana na Eddy,
askari akarusha ngumi nzito ambayo Eddy akaikwepa na kwenda kutua kwenye
kioo cha gari, hapo ikawa nafasi kwa Eddy kuanza kurusha makombora ya
ngumi mfululizo, zilizo mpata askari huyo maeneo ya kicchwani.
“POLISIIIIII”
Askari
mmoja alizungumza huku akiwa amemnyooshea bastola Edddy, wakaongezeka
askari wengine ambao walifika kwa pamoja kuifatilia gari ambayo ilimbeba
Eddy. Yote yakiwa yanaendelea Sa Yoo aliweza kuyaona kupitia juu
dirishani, kutokana akili yake kwa wakati huo haikuwa na jambo jengine
la kuwaza zaidi ya bibi yake. Hakulichukulia uzito tukio hilo la Eddy na
maaskari.
‘Siwezi kukamatwa kizembe hivi’
Eddy
akamvuta askari aliye mpiga ngumi kadhaa, zilizo mfanya aonekane kama
mlevi kwa kuyumba yumba kwake. Akampiga kabari na kuwaonya askari
wengine kwamba wakifanya jambo lolote baya mwenzao ataiaga dunia.
Kutokana aliye kabwa ni kiongozi wao hawakuwa na jinsi ya kufanya zaidi ya kuendelea kumnyooshea Eddy bastola zao.
Ukaribu
wa futi chache kutoka sehemu walipo simama askari na Eddy, ukampa
umakini wa kufikiria jambo jengine kwa haraka kujiokoa mikononi mwa
askari hao.
Akamsukumia askari aliye mkamata kwa wezake, jambo lililo wafanya askari wawili kumdaka mkuu wao asianguke chini.
Wakiwa
kwenye kurupushani ya kumdaka kiongozi wao, kipondo kikali kutoka kwa
Eddy kikaanza kutembea kwenye miili yao. Baadhi ya wananchi walio karibu
na eneo la maegesho ya magari hawakusita kuchukua video na simu zao za
mikononi kwani wengi wao walihisi ni kama mkanda wa sinema, kwa maana
mapigo ambayo askari hao wanayapokea ni kama anayopiga msanii maarufu
katika bara lao la Asia Jat Lee. Hapakuwa na mtu aliye weza kuamini
kwamba Eddy ni mwalifu, kila mmoja alisha sahau ni wapi alimuona ila
walijikuta wakifurahia tukio hilo.
Ndani
ya dakika mbili askari wote kila mmoja akawa anaugulia kivyake vyake,
Eddy akaingia kwenye moja ya gari ambalo alibahatika kukuta mlango wake
ukiwa wazi, kwa bahati nzuri zaidi akakuta funguo ya gari hilo, kwa
haraka akaliwasha na kuondoka.
Askari
hao nao wakajizoa zoa na kuingia kwenye magari yao na kuanza kumfukuzia
Eddy. Kutokana na kuto ifahamu Japan vizuri, ikamlazimu kulitekeza gari
hilo kwenye moja ya kichochoro na kuanza kukimbia kwa miguu kuelekea
asipo pafahamu.
Kutokana na mitaa mingi na idawi ya watu, askari wakajikuta wakimpoteza Eddy wasifahamu ni wapi alipo elekea.
Eddy
akafika kwenye moja ya kichochoro chenye viajana wengi wengi wanao
onekana ni wala unga na vibaka. Kutokana anajiamini sana akazidi
kukatiza katika kichochoro hicho, kila alivyo zidi kwenda ndivyo vijana
hao walivyo zidi kuongezeka nyuma yake huku wengine wakitokea kwa mbele
wakiziba njia ya yeye kupita. Huku kila mmoja akitoa kisu kwa ajili ya
kumshambulia Eddy.
***
Kila
mmoja akajikuta akiwa amemkodolea macho Rahab aliye kaa chini, kwenye
kona huku akiwa amejikunyata. Mwili mzima wa Rahab umejaa damu kuanzia
kichwani hadi miguuni. Japo na ujasiri wote wa mafunzo ya ukachero, ila
kila mmoja alijikuta akimuogopa mke wa rasisi isipo kuwa Priscar na
raisi Praygod.
“Madama”
Priscar
aliita kwa sauti ya unyonge huku akichuchumaa, akajaribu kumshika ila
Rahab akazidi kujikunja kama aneye uogopa mkono wa Priscar.
“Madam ni mimi Priscar”
Raisi
Praygod na makachero wengine wote wakawa kimya wakimsikiliza Priscar,
swali ambali lilianza kuwaumiza makachero walio mpiga risasi Rahab,
imekuwaje kuwaje hadi Rahab kuwa hai na kujikunyata katika kona hiyo,
ikiwa risasi walizo mpiga ni nyingi za kumuhatarishia maisha yake.
Kitu
kingine kilicho zidi kuwaogopesha ni viungo vya binadamu, vikiashiria
kwamba madaktari wote walio kuwa wakimfanyia oparesheni wameiaga dunia.
Rahab
akainyanyua sura yake iliyo kuwa imefunikwa na nywele zake ndefu zilizo
kuwa zimelowana damu. Akamtazama Priscar usoni, gafla machozi yakaanza
kumwagika. Taratibu rasisi Praygod akapiga magoti chini huku akiwa
hamuamini amini mke wake.
“Mke wangu”
Rahab
akamtazama raisi Praygod na kumkumbatia, wote wakajikuta wakimwagikwa
na machozi, jambo lililo wafanya makachero wengine kuwa katika hali ya
simanzi iliyo changanyikana na furaha.
Gafla
Rahab akaanza kuisikia milio ya risasi masikioni mwake, alipo nyanyua
kichwa chake akawaoa makachero walio mpiga risasi kwenye handaki. Macho
yake gafla yakabadilika na kuzidi kuwa mekundu, akamsukuma raisi
Praygod pembeni na kumrukia kachero mmoja aliye mpiga risasi, akambwaga
chini na kuanza kuliminya koo la kachero aliyeanza kutapatapa
akijitahidi kuutoa mkono mmoja wa Rahab ulio mkaba shingoni.