Jana, Jumapili Disemba 18, 2016 jijini Washington DC, Marekani
lilifanyika shindano kubwa la kumsaka Mrembo wa Dunia (Miss World 2016)
ambapo nchi mbalimbali zilishiriki kwa kuwapeleka warembo walioibuka na
ushindi katika nchi hizo.
Shindano
hilo lilimalizika kwa Mrembo kutoka nchini Puerto Rico, Stephanie Del
Valle (19) kunyakuwa taji la Mrembo wa Dunia 2016 (Miss World 2016).
Mrembo huyo alitangazwa mshindi baada ya kuwashinda warembo wengine kutoka nchi 116 duniani kote na Tanzania ikiwa moja wapo.
Mshindi
wa pili ni Yaritza Miguelina Reyes Ramirez kutoka Jamhuri ya Dominican
huku nafasi ya tatu ikiwenda kwa Natasha Mannuela kutoka Indonesia.
Hapa chini ni picha za tukio hilo lililofanyika jana.