Beki wa kushoto wa Yanga, Oscar
Joshua hatacheza katika mechi ya Kombe la Shirikisho wakati Yanga ikiivaa TP
Mazembe.
Joshua ni majeruhi baada ya kuumia
katika mechi dhidi ya Mo Bejaia nchini Algeria. Nafasi yake ilichukuliwa na
Haji Mwinyi ambaye naye alilambwa kadi nyekundu.
Kutokana na hali hiyo, Kocha Hans
van der Pluijm atalazimika kumtumia Mbuyu Twite upande wa kushoto.
Tayari Yanga ina pengo la kiungo
wake mwenye kasi, Simon Msuva ambaye ataikosa pia mechi hiyo kutokana na kuwa na
malaria.