WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amewapongeza raia wa Marekani kwa kumchagua Donald Trump kuwa rais mpya wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa Lowassa, Trump atakuwa rais mwenye kufanya uamuzi mgumu kwa kuwa ni shupavu na ana uwezo.
Trump
ambaye ni Rais Mteule wa Marekani, alichaguliwa kuwa Rais mpya wa
Marekani baada ya kumshinda mpinzani wake, Hillary Clinton, mwishoni mwa
mwaka jana.
Lowassa
aliyasema hayo jana katika misa maalumu ya shukrani ya mwaka mpya 2017
iliyoshirikisha madhehebu mawili ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT), Usharika wa Monduli na Kanisa Katoliki, wilayani
Monduli, Mkoa wa Arusha.
Ibada
hiyo, ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwamo wa Serikali na wa
vyama vya siasa, wakiwamo Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro ambaye
pia ni Katibu wa Chadema, Mkoa wa Arusha.
“Wamarekani
hawakufanya makosa kumchagua Trump kwani anaonekana kuwa na uwezo
mkubwa wa kuongoza Taifa hilo tajiri duniani ambalo linategemewa na
mataifa mengine.
“Dunia imebadilika, amechaguliwa rais mmoja huko Marekani ambaye ni mwamba kweli kweli.
“Hatuwezi
kumtabiri mambo yake yatakavyokuwa, lakini inabidi kila mtu afanye kazi
kwa bidii na kwa maarifa kwa sababu huyo hakubali upuuzi
wowote,”alisema Lowassa.
Lowassa
ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Monduli kwa miaka 20, aliwataka
wananchi kufanya kazi kwa bidii na kuacha kulalamika kwani hiyo ndiyo
njia iliyo sahihi ya kuweza kuondokana na umasikini.
“Mwaka
jana, tarehe kama hii, tulimuaga Mbunge Julius Kalanga na Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Monduli, Isack Joseph, nikawaambia nawatakia heri
wachape kazi vizuri, naona wamefanya vizuri au siyo?alihoji Lowassa.
Akizungumzia
upande wake, Lowassa alisema hivi sasa anafanya siasa za kimataifa
tofauti na siasa alizokuwa akifanya kipindi kilichopita.
“Mimi
sitaki kusema sana maana watasema napiga siasa. Siku hizi napiga siasa
za kimataifa, naomba niwatakie heri ya mwaka mpya na kila mtakachoshika,
Mungu akibariki kiwe dhahabu,”alisema