Rais
wa Zimbabwe, Robert Mugabe amepitishwa na chama chake cha Zanu- PF kuwa
mgombea urais katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo utakaofanyika mwaka
2018.
Wajumbe
wa Zanu-FP walifikia uamuzi huo wa kumpa nafasi nyingine Mugabe mwenye
umri wa miaka 92 kupitia mkutano wao uliofanyika katika mji wa kusini
mashariki wa Masvingo.
Mugabe
amelitawala taifa hilo tangu lilipopata uhuru mwaka 1980 lakini bado
chama chake kinaonesha kuwa na imani naye huku kikieleza kuwa anafaa
kuwa rais kwa maisha yake yote.
Chama
hicho kimefikia uamuzi huo wakati ambapo kumekuwa na maandamano ya
kupinga uongozi wa Mugabe kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni kupinga
anguko la kiuchumi na hali mbaya ya maisha.