TANZANIA kufikia uchumi wa viwanda mwaka 2020 kunahitajika kuwa na mazingira yatakayoweza kuwavutia wawekezaji watakaoweza kuwekeza viwanda ikiwa ni pamoja na kuimarisha viwanda vidogo vidogo katika kuzalisha bidhaa kwa wingi
Akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar,Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Sekta Binafsi Nchini (TPSF),Godfrey Simbeye ameyasema hayo wakati akitangaza mkutano wa Kimataifa uunaotarajiwa kufanyika Desemba 5 hadi 7 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Simbeye amesema kuwa mkutano huo utazishirikisha nchi mbalimbali Duniani ambazo zimepiga hatua katika sekta ya viwanda,ambapo wawekezaji watapata fursa za kuwekeza katika sekta ya viwanda nchini.
Mkutano huo ambao umeandaliwa na TPSF kwa kushiriana na tasisi mbalimbali za Serikali ikiwemo Wizara ya Viwanda,Biashara, Arusha ya International Conference Centre, Shirika la Viwanda Vidogo, Vido IDO,TIC,EPZA,ZIPA,TTB pamoja na TANTRADE ambapo kwa pamoja wataingaza Tanzania katika sekta ya viwanda nchini ili iweze kuleta matunda kwa watanzania pamoja kukuza uchumi.
Simbeye amesema mkutano kama huo ulishafanyika mara mbili katika nchi za Afrika ikiwepo Misri na Afrika Kusini na Tanzania imepata nafasi ya tatu katika kufanyika mkutano huo ambapo ni fursa ya Tanzania katika kuelekea uchumi wa viwanda kufikia 2020.
Amesema kampuni ya Biashara nchini yatafaidika katika kutanua uwigo wa mitandao ya kibiashara na kubadilishana uzoefu, taaluma za kuweza kufanya fursa za uwekezaji, kuonyesha uwepo wa nchi katika jukwaa la kimataifa pamoja na kuongeza ushawishi na kuchochea maendeleo ya kiuchumi kutokana na kuongezeka mzunguko wa fedha za kigeni nchini kutokana na ujio wa wageni wataoshiriki mkutano huo.
"Tanzania tunajivunia kuwa nchi ya tatu katika kufanyika mkutano huu, hii ni fahari sana kwetu, kwani tunaanza kuonekana kuwa nchi yetu ina hadhi” amesema Simbeye.
Sembeye amesema mikutano kama hii inapokuja katika Nchi yetu inawapa watu fursa ya kuhudhuria na kufaidika pia inasaidia kukuza uchumi kwani tunategeme kupata wageni 400 ambapo wageni 200 watatoka nje ya nchi."
Aidha ameongeza kuwa mkutano huo utakuwa sambamba na maonesho ya viwanda yatakayoanza Desemba 7 hadi 11 mwaka huu ambapo washiriki wa mkutano watapata fursa ya kutembelea maonesho hayo. Simbeye amesema Tanzania ina jumla ya viwanda 49000, lakini viwanda vikubwa vipo 2000 tu hivyo hii ni fursa kwetu kutangaza bidhaa zetu.