Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akiwa eneo la tukio-Tazama picha zaidi
AFANDE RC TAARIFA YA (M) SHINYANGA KWA SAA 12 ZILIZOPITA
06/11/2017
MAJIRA KATI YA 1900 - 1930HRS KATIKA BARABARA YA NZEGA - TINDE, KATIKA
KIJIJI CHA NSALALA KATA YA TINDE WILAYA NA MKOA WA SHINYANGA GARI NA T
232 BQR TOYOTA NOAH MALI YA MWINYI KHAMIS WA TINDE IKIENDESHWA NA SEIF
S/O MOHAMED, 32YRS, SUKUMA NA MKAZI WA TINDE, IKITOKEA NZEGA KWENDA
TINDE ILIGONGANA USO KWA USO NA SEMI TELLER T198 CBQ/T283 CBG ILIYOKUWA
IKITOKEA TINDE UELEKEO WA NZEGA MALI YA ALOYCE S/O KAVISHE, MCHAGA,
46YRS MKAZI WA DSM NA AMBAYE PIA ALIKUWA DEREVA WA GARI HILO NA
KUSABABISHA VIFO VYA WATU 18.
KATI
YAO WANAUME 7 , WANAWAKE 9 NA WATOTO 02 WAKIKE WENYE UMRI WA KATI YA
MIAKA 3- 5, MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITAL YA RUFAA YA MKOA WA
SHINYANGA.
TUKIO
HILI LIMEKAGULIWA NA ACP J. MULIRO KAMANDA MKOA WA SHINYANGA, SSP
MWAKISAMBWE - RCO SHINYANGA NA SP ANTONY MASANZU - RTO SHY AKISAIDIWA NA
DTO SHY ASP ANTONY GWANDU.
MADEREVA WOTE MBARONI KWA MAHOJIANO YA TUKIO HILO NA HATUA ZA ZAIDI ZA KISHERIA.
CHANZO
CHA AJALI HII KWA TAARIFA ZA AWALI NI UZEMBE WA DEREVA WA NOAH KUAMUA
KUYAPITA MAGARI YALIYOKO MBELE YAKE BILA KUCHUKUA TAHADHARI NA HATIMAE
KUGONGANA USO KWA USO NA LORI - SEMITELLAR. MAREHEMU WATATU
WAMETAMBULIWA.
(2) MAKOSA YA USALAMA BARABARANI YAMEKAMTWA 167, YOTE YA MELIPWA, MADUHURI YALIYOKUSANYWA TSH 4,990,000/=,
3.AFYA ZA ASKARI NA WATUMISHI RAIA KWA UJUMLA NI NZURI.
RPC SHINYANGA