Operesheni
hiyo mpya imetangazwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ikilenga
kukipa chama hicho mafanikio katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na ule
mkuu ujao.
Mbowe amesema hayo katika kikao cha uchaguzi wa mwenyekiti wa kanda wilayani Masasi mkoani Mtwara.
“Kiongozi
yeyote atakayeonyesha nia ya kutukwamisha hatutamvumilia, tutamuondoa
ili tuweze kuendelea na safari yetu na kumaliza kutembelea kanda zote,” amesema.
Amesema
ziara hizo ndizo zitakazoipa nafasi chama hicho kuchukua maeneo mengi
zaidi hasa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019.
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amesema umoja na mshikamano
ndiyo msingi imara utakaowasaidia kuweza kufikia malengo.
“Ili
kufanikiwa lazima kuwe na umoja imara baina ya viongozi wa chama. Mtu
yeyote atakayekuwa na nia mbaya na umoja huu achukuliwe hatua mara moja
ili kuepuka kutokea kwa migogoro,” amesema.
Naibu
Katibu Mkuu wa Chadema – Zanzibar, Salum Mwalimu amemshukuru Rais John
Magufuli kwa kukipa fursa adhimu chama hicho kutokana na kuzuia mikutano
ya kisiasa majukwaani jambo ambalo limewasaidia kujipanga vizuri katika
uchaguzi ujao.
“Safari
hii ni fursa kwetu, tumejipanga kiuhakika na si kwa kubahatisha
tunapoelekea katika uchaguzi wa serikali za vijiji, vitongoji, mitaa
mwaka 2019 na baadaye uchaguzi wa wabunge na Rais ifikapo 2020,” amesema.