test

Ijumaa, 11 Novemba 2016

Godbless Lema Afikishwa Mahakani...Asomewa Mashtaka Haya



Arusha. Mbunge wa Arusha mjini (Chadema), Godbless  Lema amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Lema anayekabiliwa na tuhuma za uchochezi amefikishwa mahakamani hapo kwa mapema leo (Ijumaa) asubuhi  akiwa na watuhumiwa wengine na kupelekwa moja kwa moja mahabusu akisubiri uamuzi wa mahakama  wa kupewa dhamana au la.

Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema) Joshua Nassari amesema afya ya mbunge huyo ni njema na wanasubiri mahakama ifanye uamuzi wake hapo mchana.

Kuhusu usalama Jeshi la polisi limeimarisha usalama ndani na nje ya mahakama hiyo huku wafuasi wa Chadema wakiwa katika mahakama hiyo wakisubiri hatma ya kiongozi wao.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx