Akizungumza Ijumaa hii kwenye shughuli za kutoa heshima za mwisho kwa spika huyo wa zamani wa bunge aliyefariki wiki iliyopita akiwa nchini Ujerumani kwenye matibabu, Makonda amesema wakati anasoma chuo cha Ushirika Moshi, alikosa ada ya kuendelea na masomo na kuamua kwenda kumtafuta Mzee Makamba amsaidie.
Amesema wakati akiwaeleza viongozi mbalimbali wa CCM kuhusu shida yake, alikutana na mheshimiwa Sitta ambaye baada ya kumsikiliza alimuahidi atamsomesha. Mheshimiwa Sitta alimsomesha Makonda hadi kumaliza chuo na alianza kumchukulia kama mwanae ikiwa ni pamoja na kumtambulisha kwa familia yake.
Makonda amesema Mzee Sitta aliendelea kumlea hadi kusimamia harusi yake. Anasema alijifunza mengi kutoka kwa marehemu Sitta ikiwemo tabia yake ya unyenyekevu.