test

Jumatatu, 19 Septemba 2016

Serikali yasaidia Sumbawanga walioathiriwa na mvua


Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk Halfan Haule
SERIKALI ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa imetoa msaada wa mahindi na maharage kwa waathirika walioachwa bila makazi ya kudumu baada ya nyumba 21 kubomolewa na mvua ya mawe iliyoambatana na upepo mkali.
Mvua hiyo ilinyesha juzi jioni katika kijiji cha Mtimbwa, Kata ya Kisesa, Manispaa ya Sumbawanga ikiacha familia kadhaa bila kukosa makazi na kuua mbuzi wanane, nguruwe mmoja na zaidi ya kuku 100.

Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Dk Halfan Haule alitembelea kijiji hicho na kushuhudia uharibifu uliosababishwa na mvua hiyo na kutoa msaada wa kilo 100 za mahindi na kilo 50 za maharage, huku akisisitiza wadau wengine wajitokeze kutoa misaada ya hali na mali kuwasaidia waathirika hao.
Alisema hadi sasa thamani halisi ya uharibifu uliosababishwa na mvua hiyo haijafahamika hadi hapo itakapoundwa timu ya wataalamu watakaofanya tathmini na kutoka majibu yatakayoonesha hasara halisi iliyosababishwa na mvua hiyo.
Wakizungumza na gazeti hili, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mtimbwa, Wilbroad Kapufi na Diwani wa Kisesa, Ludimila Ndinda walidai mvua hiyo iliyonyesha kwa nusu saa jana kuanzia saa 11:00 jioni ilisababisha taharuki kubwa kijijini humo.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kibori – Mtimbwa, Patrick Chula alisema kwenye kitongoji chake nyumba 12 zilibomolewa na mvua hiyo na mbuzi wanane walikufa.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx