test

Ijumaa, 16 Septemba 2016

BREAKING NEWS: WATANZANIA WALIOKUWA WAMETEKWA CONGO WAOKOLEWA



Madereva wa malori kutoka nchini Tanzania waliokuwa wametekwa katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hatimaye waokolewa na vikosi vya jeshi la nchi hiyo.Madereva hao wameokolewa usiku wa kuamkia leo baada ya mapigano makali na waasi waliokuwa wamewakamata.

Hayo ni kwa mujibu wa waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo ambaye ameiambia BBC kuwa wote wapo salama.

Mwandishi wa BBC wa eneo la mashariki mwa Congo Byobe Malenga ana taarifa zaidi.

Chanzo: BBC Swahili
Madereva wa malori kutoka Tanzania waliokuwa wametekwa katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hatimaye wameokolewa na vikosi vya jeshi la nchi hiyo.

Waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo amezungumza na shirika la utangazaji la BBC na kusema wote wameokolewa   na wako salama

Taarifa iliyotolewa jana  na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilieleza kuwa watekaji hao ni kikundi cha waasi cha MaiMai ambao baada ya kuyateka magari 8 toka Tanzania , waliwashusha madereva na kuwapeleka porini na kisha kuteketeza kwa moto malori manne ambayo yote ni ya Bw. Dewji. 

Waasi hao walitoa saa 24 kuanzia jana saa 10 jioni walipwe fedha kiasi cha Dola za Kimarekani 4,000 kwa kila dereva ili waweze kuwaachia.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx