Mwanadada anayeuza sura kwenye video mbalimbali za wasanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ ameibuka na kusema kuwa kitendo cha Mwanamuziki Esterlina Sanga ‘Linah’ kuamua kumchukua mpenzi wake, Idris Sultan ni dhahiri kwamba anafanya malipizi hivyo kamwe hatamvumilia.
Mwanamuziki Esterlina Sanga ‘Linah’
Akichonga Gigy Money ambaye awali aliingia kwenye vita ya maneno na Mwigizaji Wema Sepetu baada ya kumkwapulia bwana (Idris), alisema Linah amelipiza kisasi kwa kuwa aliwahi kumchukulia mpenzi wake, Billnas ila anafanya juu chini mpaka amrudishe Idris kwenye himaya yake.
Mwanamuziki Esterlina Sanga ‘Linah’
“Linah ameamua kulipa kisasi baada ya mimi kutembea na aliyekuwa mpenzi wake, Billnas ambaye niliona hajui mapenzi nikaamua kumpiga chini, sasa huu moto ndiyo umewaka, yule hawezi kushindana na mimi, anisikilizie tu atajua mimi ni nani kwanza Idris lazima nimrudishe kwenye himaya yangu,” alisema Gigy Money.
Gift Stanford ‘Gigy Money’
Baada ya Gigy kuweka wazi hayo, gazeti hili lilimtafuta Linah ili kujibu tuhuma hizo lakini simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno kwenye Mtandao wa Kijamii wa WhatsApp hakujibu chochote licha ya kuonesha kwamba ameusoma