test

Alhamisi, 11 Agosti 2016

Waziri wa Habari, Utamaduni. Sanaa na Michezo nchini, Nape Moses Nnauye ametoa tahadhari kwa waandishi na vyombo vya habari


Nape Nnauye


Hiyo ni taarifa kutoka kwa Waziri wa Habari na Utamaduni, Nape Nnauye kwenda kwenye vyombo vyote vya habari nchini....


Chanzo: Magic Fm
============

Waziri wa Habari, Utamaduni. Sanaa na Michezo nchini, Nape Moses Nnauye ametoa tahadhari kwa waandishi na vyombo vya habari ambavyo vitajihusisha na kuripoti mikutano, maandamano au habari yoyote ambayo ni ya kichochezi kwa taifa kuwa vitahesabika kuwa vyenyewe navyo ni vya kichochezi, hivyo chombo husika kinaweza kufungiwa kwa kueneza uchochezi.

Amesema vyombo vya habari havipaswi kuripoti habari za kuonyesha kuichonganisha serikali na wananchi wake.

Hayo yamesemwa wakati wa kumtambulisha ndugu Hassani Abbas aliyechukua nafasi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Habari-Ikulu (Msemaji wa Serikali), Assah Mwambene.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx