Wanafunzi
wa Zanzibar wanaosoma katika vyuo vikuu viliopo bara na Zanzibar
wamevamia Ofisi za bodi ya mikopo ya Zanzibar wakidai posho zao ambazo
hawajalipwa kwa kipindi cha mwaka mzima na fedha za ada za masomo.
ITV iliwakuta wanafunzi hao wapatao 70 wamekusnayika nje ya jengo
la bodi hiyo ya mikopo wakitafakari na kutafuta mbinu za kudai
malimbikizo ya fedha zao za posho ambazo ni zaidi ya mwka mzima
hawaajlipwa na bodi hiyo imekuwa ikitoa ahadi hewa kupata fedha hio na
wameiomba seriklai ilivalie njuga suala hilo.
Hata hivyo ITV ilipamta mkurugenzi mkuu wa bodi hiyo ya mikopo ya
Zanzibar Bw.Idi Khamis ambaye amekiri kuwepo kwa hali hiyo ya wafaunzi
inagawa amesema tatizo kubwa linakuja kuwa wanafunzi hao wnyewe hawalipi
madeni yao ambapo wanadai karibu bilioni 30 huku akiwahakikishia
wanfunzi hao pamoja kuwa serikali tayari imeshandaa mpango wa kulipa ada
mwaka huu wanapaswakueelewa kuwa sio bodi ndio yenye malaka ya kulipa
fedha zote..
Bodi hiyo ya mikopo ya zanzibar ambayo hutegemea ruzuku serikalini
na fedha za urejeshaji inahitaji shlingi bilioni 8 kwa mwaka kwaajili
ya kuwalipia ada na posha wanafunzi wanaosoma Tanzania bara katika vyuo
mbali mbali na wakiwemo wanfunzi wa Zanzibar walioko hapa.
0 comments:
Chapisha Maoni