Malalamiko hayo wameyatoa kwa katibu mkuu wa usimamizi wa makampuni
ya uchimbaji wa madini nchini(TAMICO) Bw.Hassani Amir na kudai licha ya
mgodi huo kutembelewa hivi karibunina waziri mwenye dhamana Bw.George
Simba Chawene na kutoa malalamiko yao bila ya mafanikio huku wakishindwa
kumtambua mkurugenzi wa kampuni hiyo kwa kuwa hajawahi kukutana na
wafanyakazi hao tangu aliporithi toka kwa mwekezaji wa nje hali
inayowanyima maslahi yao stahiki na kushindwa nani anastahili kuwalipa.
Hata hivyo katibu mkuu wa Tamico Bw.Hasani Amiri licha ya kupokea
malalamiko ya wafanyakazi hao alipata wakati mgumu wa kukutana na
uongozi wa kampuni hiyo ambao haukuhudhuria kikao hicho huku afisa
mwajiri Bw.Kirani Laiza alipotakiwa kutoa maelezo alionekana kushindwa
kutoa maelezo akidai wafanyakazi hao walimkata mtu mmoja aliyefahamika
kwa jina la Anthony Kukaimu nafasi hiyo.
Akitoa hitimisho kwa wafanyakazi hao huku akiwataka kuacha kugoma
na badala yake akiahidi kutatua mgogoro huo ikiwa ni pamoja na kuipeleka
kampuni hiyo mahakamani kwa kuwa imekiuka makubaliano ya awali kwa
kuvunja sheria za wafanyakazi wa Migodini.
0 comments:
Chapisha Maoni