Mgombea
urais wa vyama vinavyounda UKAWA Mh.Edward Lowassa amesema
akichaguliwa kuwa rais hatakuwa na sababu ya kutegemea misaada kutoka
nje kutekeleza ahadi anazotoa na sera zilizoko kwenye ilani ya UKAWa
badala yake atasimamia vizuri rasilimali zilizopo kwani zinatosha
kutatua matatizo ya watanzania.
Baada ya kumaliza kazi ya kufikisha ujumbe wa mabadiliko kwa
wananchi wa mkoa wa Dodoma ambao ni ngome na pia makao makuu ya CCM
kwa mafanikio makubwa Mh.Lowasa anaingia kwa kishindo katika mkoa wa
Singida na kupokelewa na umati wa wananchi wakiwa na matumaini
makubwa ya kupata mabadiliko ya maisha yao kupitia ukawa chini ya
Mh.Lowasa,ambaye amewaomba kumpa nafasi ya kushughulikia kero zao kwani
anazijua na asilimia kubwa ufumbuzi wake uko ndani ya uwezo wake.
Mh.Lowasa ambaye awali amefanya mikutano katika wilaya ya
Manyoni,Ikungi na Singida mjini anasema kupitia sera zilizoko kwenye
ilani ya UKAWA na uwezo mkubwa wa viongozi na watendaji wana kila
sababu ya kubadilisha maisha ya watanzania kwa muda mfupi na kwa
ufanisi mkubwa.
Baadhi ya wananchi na viongozi wanaounga mkono mabadiliko wamesema
ubora wa sera zilizoko kwenye ilani ya UKAWA kugusa matatizo ya
watanzania,UKAWA inaendelea kuwa kimbilio la,wananchi na viongozi
wakiwemo wanaotoka CCM huku wakiendelea kuwaeleza wananchi faida za
kubadilika na athari za kuendelea kuvumilia mateso ya CCM na ahadi
zinazoonekana wazi kuwa hazitekelezeki.
0 comments:
Chapisha Maoni