Rais
wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dakta Jakaya Mrisho Kikwete
ameiagiza idara ya mambo ya kale kushirikiana na mamlaka ya hifadhi ya
Ngorongoro kuhakikisha kuwa eneo la laitoli zinapopatikana nyayo za mtu
wa kale anayesadikiwa kuwa binadamu wa kwanza linahifadhiwa kitaalamu .
Dakta Kikwete anatoa agizo hilo jijini Arusha katika hafla ya
uwekaji wa jiwe la msingi la jengo la kitega uchumi la mamlaka ya
hifadhi Ngorongoro na kuongeza kuwa hifadhi ya eneo hilo itaongeza idadi
ya watalii wanaoingia kuona maajabu ya Ngorngoro.
Awali akioa taarifa ya ujenzi wa jengo hilo linalokadiriwa kuwa na
ghorofa kumi na tano,mwenyekiti wa bodi ya mamlaka ya Ngorongoro balozi
Mwanaidi Maajar aamesema lengo la ujenzi wa kitega uchumi hicho ni
kuiwezesha mamlaka kuongeza vyanzo vya mapato nje ya mapato yatokanayo
na utalii.
Na hatimaye bodi ya mamlaka ya Ngorongoro na baraza la wafugaji
wakatumia fursa hiyo kumuaga rasmi rais Kikwete kwa kumpatia zawadi
mbalimbali kikiwemo cheti cha kutambua mchango wake kwenye kutangaza
utalii.
0 comments:
Chapisha Maoni