Watu wawili, mke na mume wakazi wa Makambo, wilayani Mlele, wameuawa kikatili kwa kuchinjwa na kutenganishwa kichwa na kiwiliwili wakati wakiwa wamelala.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, aliwataja wanandoa
hao kuwa ni Seth Mwakalimbwa (65) na Yakoba Kalulu (48).
Kidavashari
aliwaambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo lilitokea Mei 21, usiku
nyumbani kwa wanandoa hao ambao baada ya kuuawa miili yao iliachwa
kitandani.
Alisema marehemu hao wakati wa uhai wao walikuwa wakiishi kwenye nyumba yao peke yao kwa muda mrefu.
Alisema,
balozi wa eneo hilo, Wilbroad Mahenge, ndiye aliyegundua vifo hivyo
baada ya kutowaona wanandoa hao kwa siku mbili mfululizo na kuingiwa na
wasiwasi.
Kamanda
Kidavashari alisema balozi huyo aliamua kwenda kwenye nyumba ya
wanandoa hao ili kujua hali zao na alipofika alikuta milango ikiwa wazi
hali iliyosababisha apate mashaka.
Alisema
alijaribu kuwaita kwa majina yao lakini hakuna aliyeitika na aliamua
kuingia ndani na kuwakuta wakiwa wamelazwa kitandani huku wakiwa
wamefariki dunia kwa kuchinjwa shingo zao na kutenganishwa kiwiliwili na
kichwa.
Alisema, balozi Wilbroad alikwenda kutoa taarifa kwenye uongozi wa serikali ya kitongoji ambao nao walitoa taarifa polisi.
Kamanda alisema chanzo cha mauaji hayo ni imani za kishirikina.
Aidha, alisema mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.
Alisema
polisi kwa kushirikiana na uongozi na wanakijiji wa Makambo,
wanaendelea na msako ili kuwabaini watu waliohusika katika mauaji hayo.
0 comments:
Chapisha Maoni