Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wilayani Songea jana limezua
kizaa zaa kwa wananchi kufuatia kuvamia mitaani, maofisini (serikali na
binafsi) makanisani na misikitini wakiwa na silaha huku magari yao
yakiranda kila kona na kuanza upekuzi kwa watu wote walokutana nao huku
wakidai kuonyeshwa vitambulisho.
Aidha,indaiwa kuwa baadhi ya wakazi wa mjini hapo waliamua kujifungia
ndani huku wengine wakisema kwamba jeshi hilo linawasaka magaidi
waliovamia katika mji wa Songea kutokana na jeshi hilo kutowafahamisha
wananchi nini hasa dhumuni la msako huo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela
alipoulizwa alisema zoezi hilo ni la kawaida huku akiwataka wakazi wa
mjini songea kuwa na amani na waendelee kufanya shughuli zao kama
kawaida.
Naye Brigedia Jenerali wa Kamandi ya Kusini, John Chacha alisema
hiyo ni sehemu ya mafunzo kwa wanajeshi hao na kuongeza kuwa jeshi
hilo hufanya mafunzo mbalimbali ya kujiimarisha ikiwamo ya kulinda
miji, maporini na mengineyo.
0 comments:
Chapisha Maoni