Bosi huyo toka ureno atakua makini sana katika mipango yake kuhakikisha the blues wanatetea ubingwa wao msimu ujao.
Lakini sheria mpya ya matumizi ya fedha ya UEFA {Financial Fair Play}itawabana kwa hiyo matajiri hao kutoka London ya kaskazini watatakiwa kuuza wachezaji wawili au watatu ili waweze kununua wachezaji wengine kuongeza kikosi chao.
Kwa hiyo nani msimu huu ataondoka Chelsea ili usajili mpya ukamilike?hebu tuangalie wachezaji watano ambao wakiuzwa wanaweza kuingiza kipato cha hadi paundi million 70 ili kuwezesha usajili mpya.
Namba 5 ni Filipe Luis,alisajiliwa kama mrithi wa Ashley Cole msimu uliopita,lakini mbrazil huyo ameshindwa kupata namba mbele ya mhispania Cesal Azpilicueta,japokua walitumia paundi million 15.8,Anaweza kurudi katika klabu yake ya zamani ya atletico Madrid na mapato yake yakamsaidia Jose Mourinho kumsajili kiungo mkabaji Koke.
Namba 4 ni mbrazil mwingine Oscar,japokua alianza vizuri sana chini ya Benitez na alikua moja ya nyota wa kutegemewa sana pale darajani lakini kiungo huyo mshambuliaji ambae amefunga na kutoa pasi nyingi tu za magoli msimu huu alijikuta mvuto wake kwa kocha mourinho ukipungua kiasi cha kumfanyia mabadiliko mara kwa mara au kukaa benchi kabisa.akiwa na miaka 23 tu anaweza kuwa mmoja wa wachezaji watakaojikuta nje ya Chelsea msimu ujao.
John Mikel Obi,Nyota huyu wa Nigeria amejikua akipotezwa kabisa na ujio wa Nemanja Matic pamoja na uwepo wa Ramires na Kurt Zouma katika nafasi ya kiungo mkabaji,wakati huo kinda mwingine kutoka akademi ya Ruben Loftus anaweza kuanza kuitumikia klabu hiyo muda si mrefu,kuondoka kwake kutaipunguzia mzigo klabu yake hasa kutokana na mshahara wake mkubwa na wanaweza pata pesa nzuri kutokana na mauzo yake.
Petr Cech,alisajiliwa na Jose Mourinho mwenyewe na amekua nguzo muhimu sana pale darajani lakini ujio wa Thibaut Courtouis na fomu nzuri aliyoionyesha kwa kuruhusu goli moja tu katima mechi sita za ugenini walizocheza,kwa bahati mbaya Cech hatotaka kuwa katika bench msimu ujao na anaweza kuuzwa kwa paundi million 7 hadi 10.
Namba 1,ni Mohamed Salah, baada ya kushindwa kumshawishi kocha wake baadaya kusajiliwa toka fc basel kwa kitita cha paundi million 11,nyota huyo toka misri ambae yupo kwa mkopo pale Fiorentina akiwa na magoli manne na pasi moja ya goli katika michezo 12,hilo limamfanya awe rahis kuuzika katika dirisha la usajili litakapo funguliwa.
0 comments:
Chapisha Maoni