Rais Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Mzee Joseph Mungai, aliewahi kuwa Waziri katika Wizara mbalimbali za Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuanzia Awamu ya kwanza mpaka ya nne, ulioagwa leo katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole mjane wa Marehemu Mzee Joseph Mungai.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin Mkapa akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Mzee Joseph Mungai, aliewahi kuwa Waziri katika Wizara mbalimbali za Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuanzia Awamu ya kwanza mpaka ya nne, ulioagwa leo katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohamed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Mzee Joseph Mungai, aliewahi kuwa Waziri katika Wizara mbalimbali za Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuanzia Awamu ya kwanza mpaka ya nne, ulioagwa leo katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli (wa nne kushoto), Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin Mkapa (wa tatu kushoto), Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohamed Gharib Bilal (wa tatu kulia), Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye (kushoto), Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mama Salma Kikwete (kulia) pamoja na viongozi wengine wakifatilia wasifu wa Marehemu Mzee Mungai, uliokuwa ukisomwa na Mtoto wake Mkubwa, Jimmy Mungai.