Na Dotto Mwaibale
KUNDI
la uhalifu la watoto wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 25 maarufu kama
panya road linatishia usalama wa wananchi na mali zao maeneo ya Moshi
Baa na vitongoji vingine katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Kufuatia
kukithiri kwa vitendo hivyo katika kipindi kisichopungua wiki mbili
tayari watoto watatu walikuwa wakidaiwa kuhusika na kundi hilo wameuawa
na wananchi wenye hasira kali.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hii Dar es Salaa jana mkazi wa eneo la Moshi
Baa Relini aliyejitambulisha kwa jina la Mwarami Abubakar alisema hali
sio shwari katika eneo kufuatia matukio ya kila siku ya kuvamiwa
wananchi kujeruhiwa na kuporwa mali zao na kundi hilo.
"Tayari
vijana wawili wiki iliyopita wamechomwa moto na wananchi wenye hasira
huku mwingine akipigwa juzi hadi kutolewa utumbo na kufariki papo hapo,"
alisema Abubakar.
Mkazi
mwingine wa eneo la Kwa Mkolemba Khamisi Fadhil alisema kundi hilo
limekuwa likifanya vitendo hivyo mchana kweupe na wanatembea kuanzia
vijana nane hadi 10 wakiwa na silaha za jadi kama nondo, visu na mapanga
na mtu yeyote wanayekutana naye ni lazima wampige na kumpora.
Wenye
maduka wanalazimika kufunga kuanzia saa moja jioni kuhofia kundi hilo
ambalo huvunja milango ya nyumba na kufanya uporaji" alisema Fadhil.
Fadhil alisema maeneo ambayo vijana hao wameshamiri ni Moshi Baa Relini, Kwa Mkolemba, Diwani na Bomba mbili.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Kamishna Msaidizi (ACP), Salum
Hamdan alisema polisi imejipanga vilivyokukabiliana na vitendo hivyo
katika mkoa wake.
"Kwanza
napenda kukuambia kwamba hakuna kundi linalojiita panya road wote
tunawahesabu ni wahalifu kama walivyo wahalifu wengine na hivi
ninavyongea na wewe tupo katika siku ya sita ya operesheni ya kukakamta
watu wanaojihusisha na uhalifu wa ujambazi wakiwemo wanaouza pombe
haramu ya gongo," alisema Kamanda Hamdan.
Aliongeza
kuwa katika mkoa wake hivi karibuni utakuwa shwari baada ya askari wake
kusambaratisha watu hao wanaofanya vitendo hivyo.
Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062