test

Jumamosi, 9 Mei 2015

LIST MPYA : HAWA NDIO WASANII WA HIP HOP 5 WENYE PESA NYINGI DUNIANI NA CONNECTION ZAO KWENYE MICHEZO


peaa
It’s all about the Benjamiz na bado wanaendelea kuzitaguta hawa jamaa watano. Wana nguvu sana kwenye muziki wa Hiphop na wametajwa na forbes.com kwamba ndio wanapesa nyingi kuliko wasanii wengine wote kwenye muziki wa Hiphop.
Kwenye hii story pia utajua connection yao kwenye sports

b2
  1. Sean Diddy Combs “P.Diddy” – $735 Million
Diddy ameendelea kuongoza list ya wasanii wa Hiphop wenye pesa nyingi duniani. Vyanzo vya pesa za huyu jamaa ni kutokana na clothing line yake ya Sean John ambapo hivi sasa ame-launch perfume mpya inatwa 3AM. Brand ya maji Aquahydrate ambayo yalikua official water ya Manny Pac kwenye MayPac. Vyanzo vikubwa vya pesa za Diddy ni Ciroc Vodka pamoja na DeLeon tequila chini ya kampuni yake ya Combs Wines and Spirits akishirikiana na kampuni kubwa duniani ya vinywaji Diageo.
Diddy anategemewa kuendelea kupanda juu kwasababu hivi sasa TV network yake ya Revolt inafanya vizuri sana nab ado ana investment nyingine mbalimbali kama Blue Flame Angency,Bad Boy Record Label  na nyingine nyingi.
Kwenye michezo Diddy aliwai kuhusishwa na tetesi za kutaka kuwekeza kwa kiasi kikubwa kwenye timu ya Crystal Palace wakati ipo ligi kuu.

b5
  1. Dre – $700 million
Alitegemewa kuwa bilionea wa kwanza kwenye Hiphop lakini haijawa hivyo. Baada ya kuuza brand ya Beats by Dre kwa kampuni ya Apple pesa alizopata zimempa boost ya kufika namba mbili lakini sio juu ya Harlem boy P Diddy.
Lakini Dr Dre ameweka historia kwa wasanii wa Hiphop kwasababu alipata pay ya ghafla na kuongeze net worth yake tofauti ya wasanii wengine ambao ilibidi wasubili miaka kupiga pesa alizokamata Dr Dre.

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/05/b3.jpg
  1. Jay Z – $550 million
Jay Z anatabiliwa kufanya vizuri kwenye miaka ijayo kwasababu ya kuzindua mtandao wake ambao unafanya kazi ya online streaming ya music unaitwa Tidal. Uwekezaji wa kwenye internet siku zote huwa unalipa kwa haraka na kiasi kikubwa sana.
Lakini pesa hizi za sasa hivi za Jay zinatokana na mgawanyiko wa uwekezaji chini ya kampuni yake ya Roc Nation. Label yake inawasanii wanaofanya vizuri sokoni na pia anawekeza kwenye michezo na Roc Nation Sports. Jay Z anamsimamia wachezaji maarufu kwenye NBA,NFL na michezo mingine kama MVP wa NBA 2013/2014 Kevin Durant na mchezaji WNBA Skylar Diggins.
Vitu vingine ni Armand de Brignac Champagne,Club za 40/40 na vitu vingine mbalimbali. Kwenye michezo Jay Z alihusishwa kuhusu uwekezaji kwenye club ya Arsenal lakini hivi sasa anategemewa kuwa partner wa David Beckham kuanzisha timu ya soccer USA.

b4
  1. 50 Cent – $155 miilion
Kwenye music 50 Cent hajatoka miaka mingi sana iliyopita ukifanisha na wenzake ambao wapo kwenye top 5 lakini amefanikiwa ku-make pesa nyingi sana kwa muda huo mfupi.
Baada ya kupiga $100 milion baada ya kuuza Vitamin water mwaka 2007, 50 Cent anategemea kupiga pesa nyingi kwenye uwekezaji wake mpya kutoka kwenye SMS headphones,Effen Vodka na Frigo underwear.

b

  1. Birdman – $150 million
Huyu jamaa ameshuka kidogo kutoka $160 million kwa mwaka jana hadi hadi mwaka huu. Pia tetesi za kutaka kuondoka kwa wasanii wakubwa kwenye label yake kama Lil Wayne inaweza kusababisha akashuka Zaidi mwakani

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni