Licha
ya jitihada zilizofanywa na Naibu Waziri wa Afya na Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma kuwatuliza wanafunzi wa kitivo cha elimu wasigome na kwamba
Serikali itafanya kila jitihada kuhakikisha wanapata fedha hizo kwa
haraka, jitihada hizo hazijazaa matunda kwani wanafunzi walisisitiza
wataendelea na mgomo wao mpaka pale watakapolipwa fedha zao sababu hawawezi kusoma wakiwa na njaa na imekuwa kawaida ya serikali kuwadanganya.
Leo hali imekuwa ni tete zaidi baada ya mgomo wa
kususia
masomo Chuo Kikuu cha Dodoma kuendelea kushika kasi. Majira ya saa nne
asubuhi hali imeendelea kuwa mbaya zaidi huku wanafunzi wakihitaji
kuelekea utawala Mkuu wa Chuo ili kuitiwa Waziri Mkuu wa Nchi, Mh;
Pinda.
Baada
ya muda mfupi hali ilichafuka na askari wwakaanza kushambulia kwa
kuwatawanya wanafunzi, huku wakiwataka warudi mabwenini kwao.
0 comments:
Chapisha Maoni