Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) limethibitisha kupokea barua ya Yanga yenye ombi
la kujiondoa kwenye mashindano ya Kagame Cup yanayotarajia kuanza Juni
29 mpaka Julai 13 2018.
Kwa
mujibu wa Ofisa wa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo, amesema wamepokea
barua hiyo inayoeleza kuwa Yanga ina nia ya kuwapa mapumziko wachezaji
wake.
Barua
hiyo iliyowasili katika makao makuu ya TFF, imesema Yanga inahitaji
kuwapa muda wa kupumzika wachezaji wake kwa ajili ya mashindano ya Kombe
la Shirikisho Afrika.
Yanga
itakuwa ina kibarua kizito kitakachopigwa nchini Kenya dhidi ya
mabingwa wa ligi nchini humo kwa msimu wa 2017/18, Gor Mahia FC Julai
18.
Kutokana
na muingiliano wa ratiba hiyo ya Kagame na CAF, Yanga wameona ni vema
zaidi kuwapa wachezaji wake mapumziko ili kujiandaa kuelekea mechi hiyo
ya kimataifa.
0 comments:
Chapisha Maoni