Waziri
wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema ahadi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) ya kutoa Sh50 milioni kila kijiji itaanza kutekelezwa
mara baada ya mfumo wa kuanza kuzitoa utakapokamilika.
Dk
Mpango ametoa kauli hiyo jana jioni bungeni wakati akijibu hoja ya
Mbunge wa Karagwe (CCM), Innocent Bashungwa aliyoitoa wakati Bunge
likiwa limekaa kama kamati kupitia vifungu kwa vifungu vya Bajeti ya
Wizara ya Fedha na Mipango ya mwaka 2018/19.
Bashungwa
alisema, “Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020, tulitoa ahadi ya kutoa Sh50
milioni kila kijiji.” “Bajeti ya mwaka 2016/17 ilitengwa Sh60 bilioni na
mwaka 2017/18 ilitenga Sh60 bilioni lakini mpaka sasa hazijaenda,
nataka kujua kwa nini hazijaenda?”
Akijibu
hoja hiyo, Dk Mpango alisema, “ni kweli jambo hili ni ahadi ya chama na
ninaomba nikumbushe kwamba ni ahadi ya chama kwa kipindi cha miaka
mitano.
0 comments:
Chapisha Maoni