Ameagiza
kutafutwa na kukamatwa kwa mwalimu huyo anayetuhumiwa kufanya vitendo
hivyo ambaye tangu Machi 16, 2018 haonekani shuleni hapo.
Tangu
jana jioni kumekuwa na taarifa za mwalimu mmoja wa shule hiyo
kuwanajisi watoto wanne wa darasa la saba, jambo lililozua taharuki.
Mkuu
huyo wa wilaya alipowasili shuleni hapo alipokewa na mwalimu mkuu,
Wilson Mwabuka huku baadhi ya walimu wakitimua mbio na kujifungia
wakihofia kupigwa picha.
Akizungumza baada ya kutembelea shule hiyo, Hapi aliwataka wazazi na jamii kuwa watulivu wakati polisi wakiendelea na uchunguzi.
"Walimu,
wanafunzi na watumishi wa shule ni binadamu na kila binadamu ana hulka
zake ndio maana tunazo sheria kwa kuwa makosa hayawezi kutotokea. Makosa
ya walimu yasichanganywe na makosa ya taasisi, tuiache taasisi iendelee
kutoa elimu," amesema.
Awali, Mwabuka alisema tayari Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi hivyo hataweza kuzungumzia jambo hilo.
Amesema tangu Machi16, 2018 mwalimu huyo hajaonekana shuleni.
"Kwa
hiyo kwa sababu mimi siyo mwanasheria siwezi kuzungumza, nawaomba
wazazi na jamii kusubiri polisi kwa sababu wanaendelea kufanya uchunguzi
na wameshatuhoji," amesema.
0 comments:
Chapisha Maoni