Wakongwe
wa soka Tanzania, Simba SC na Yanga SC wamepangwa Kundi C katika
michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Kagame Cup
inayotarajiwa kuanza Juni 28 hadi Julai 13 mwaka huu mjini Dar es
Salaam.
Akitaja
makundi ya michuano hiyo, Katibu wa kudumu wa Baraza la Vyama vya Soka
Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye alisema kwamba
pamoja na Simba na Yanga, timu nyingine katika Kundi hilo ni Dakadaha ya
Somalia na Saint George ya Ethiopia.
Musonye
alisema kwamba Kundi A linaundwa na timu za Azam FC, KCCA ya Uganda,
JKU ya Zanzibar na Kator FC wa Sudan Kusini, wakati Kundi B linaundwa na
timu za Rayon Sport ya Rwanda, Gor Mahia ya Kenya, Lydia Ludic ya
Burundi na Ports ya Djibouti. Musonye aliishukuru Tanzania kwa kukubali
kuwa wenyeji wa michuano hiyo na akasema kwamba anatarajia itafana kwa
sababu ya rekodi ya nchi hii kuandaa mashindano yaliyokuwa na msisimko
mkubwa miaka ya nyuma.
Musonye
ambaye alisema mashindano yatafanyika viwanja vya Taifa na Azam
Complex, Chamazi – pia amewapongeza Rwanda na Rais wao, Paul Kagame kwa
kuwa wadhamini wa mashindano haya kwa zaidi ya miongo miwili sasa.
Musonye
amesema kwamba wamelazimika kufanya mashindano ya mwaka huu sambamba na
Fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi, kwa sababu wasipofanya mwezi
huu hayatafanyika tena kwa mwaka wa tatu mfululizo.
Hata
hivyo, Musonye amesema kwamba watatoa ratiba nzuri ambayo haitaruhusu
mashindano ya mwaka huu kuingiliana na mechi za Kombe la Dunia.
Kwa
upande wake, Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Tido Mhando alisema
kwamba wataitumia michuano hiyo kukizindua kituo chao chao Redio, Uhai
FM na akawahakikishia kwamba pamoja na mashindano hayo kufanyika
sambamba na Kombe la Dunia, lakini yatafana
FIFA
imeridhia Kagame kufanyika mwezi huu tofauti na agizo lake la kutotaka
katika mwezi wa Fainali za Kombe la Dunia yasifanyike mashindano mengine
yoyote, kwa sababu washiriki watano wa michuano hiyo wapo kwenye hatua
ya makundi ya michuano ya Afrika, ambayo kwa sasa imesimama kupisha
Kombe la Dunia itarejea Julai baada ya kumalizika kwa michuano hiyo
nchini Urusi.
Hao
ni KCCA ya Uganda iliyopo Kundi A katika Ligi ya Mabingwa Afrika na
nyingine nne kwenye Kombe la Shirikisho ambazo ni Gor Mahia ya Kenya,
Rayon Sports ya Rwanda, Yanga ya Tanzania zilizopoi Kundi D zote na
Al-Hilal ya Sudan iliyopo Kundi A.
Na
kwa sababu hatua ya makundi ya michuano hiyo ya Afrika itakwenda hadi
Agosti, mwezi ambao msimu mpya wa Ligi Kuu nyingi duniani huanza –
michuano ya Kagame isipofanyika mwezi huu kuna hatari isifanyike tena na
mwaka huu kwa mara ya tatu mfululizo.
Azam
FC ndiyo mabingwa wa mwisho wa michuano hiyo ilipofanyika Tanzania,
walipowafunga Gor Mahia 2-0 katika fainali Uwanja wa Taifa mjini Dar es
Salaam, mabao ya waliokuwa washambuliaji wake hatari, John Raphael Bocco
dakika ya 17 na Muivory Coast, Kipre Herman Tchetche dakika ya 64.
Na
hiyo ndiyo ilikuwa michuano iliyomtoa mshambuliaji Mkenya, Michael
Olunga ambaye kwa sasa anachezea Girona FC ya Hispania kwa mkopo kutoka
Guizhou Zhicheng ya China.
Baada
ya kufungha mabao matano akiwa na Gor Mahia na kuibuka mfungaji bora
akiwapiku , Osman Bilal Salaheldin wa Al-Khartoum ya Sudan aliyefunga
mabao manne sawa na Tchetche wa Azam FC, Olunga akachukuliwa na
Djurgardens IF ya Sweden mwaka 2016 iliyomuuza Guizhou Zhicheng mwaka
2017.
Na Tanzania itawakilishwa na Azam FC kama mabingwa watetezi wa mashindano na Yanga SC, kama mabingwa wa nchi.
Credit: Full Shangwe
Credit: Full Shangwe
0 comments:
Chapisha Maoni