Rais
Dkt. John Magufuli amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon
Sirro kuhakikisha inapofika kesho (Aprili 8, 2018) awe ameshawaingiza
askari Polisi walionguliwa nyumba zao hapo awali katika nyumba mpya
ambazo zimezinduliwa hii leo.
Dkt.
Magufuli ametoa agizo hilo leo (Aprili 7, 2018) wakati alipokuwa
anazungumza muda mchache alipomaliza kuzindua nyumba za askari
zilizojengwa mkoani Arusha na kusema anawapa pole kwa majanga
yaliyotokea ya kuunguliwa moto, huku akiwapongeza wadau mbali mbali
waliojitolea kwa mioyo yao katika ujenzi wa nyumba hizo.
"Nimepata
mawazo ni kitu gani tunaweza kufanya kuhusina na matatizo ya nyumba za
Polisi, sasa ninachoomba Mhe. IGP wale walionguliwa nyumba, kesho
waingie katika nyumba zao hizi mpya ambazo zimemalizwa kujengwa.
Kwasababu najua muda mwingine wanaweza wakachomekwa Polisi wengine
halafu waliokuwemo wakaambiwa hapana", amesema Dkt. Magufuli.
Pamoja
na hayo, Rais Magufulia ameendelea kwa kusema "sasa nataka wale wale
walionguliwa ndio waingie humo kwenye nyumba kwasababu Mungu
aliwasaidia, moto ukaungua ungua kwa faida ya wao lakini hii
inadhihirisha ni kwa namnagani makazi ya nyumba za polisi yalivyo kuwa
mabovu"..


0 comments:
Chapisha Maoni